fbpx

Simu rununu Realme 2 Pro imetoka

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Ushindani kwenye biashara ya simu janja bado unaendelea kwa kuwa kila leo kuana simu rununu inatoka na kuiweka kampuni husika kutengeneza faida kutokana na bidhaa husika ikiwemo Realme 2 Pro.

Oppo inafamika ulimwenguni kwa vitu vyao na pengine ulikuwa ufahamu kuwa mbali na kutoa bidhaa zinazobeba nembo ya Oppo lakini kuna vitu vingine vinatoka mathalani Realme 2 Pro huku kampuni mama ni Oppo. Naamini unataka kujua simu hiyo ina sifa gani:

Kipuri mama+Muonekano.

Simu husika inatumia  Snapdragon 660 ambayo ni moja ya vipuri mama ambavyo vina kasi na kuifanya simu kuvutia wakati wote. Kioo chake kina urefu wa inchi 6.3 kiwango cha ung’avu wa hali ya juu.

INAYOHUSIANA  Google kuendelea kushirikiana na Huawei kwa siku 90 zijazo

Kamera.

Realme 2 Pro ina kamera mbili upande wa nyuma; za MP 16 na nyingine 2 MP. Kwa mbele ipo kamera moja tu lakini ambacho kimenivutia ni ule muonekano wake.

Realme 2 Pro

Kamera ya mbele kwenye Realme 2 Pro MP 16 lakini pia ule mtindo wa simu kuwa na umbo la herufi “V” umewekwa kwenye kamera ya mbele.

Memori ya ndani+RAM.

Kipengele hiki kimenivutia sana hasa kutokana na aina tofauti tifauti za ukubwa wa memori; kuna yenye RAM GB/64GB diski uhifadhi, 6GB RAM/64GB memori ya ndani na GB 8 za RAM/128GB diski uhifadhi.

Betri+Programu endeshi.

Katika moja ya vipengele ambavyo huwa napenda kuvitolea macho kwa ukaribu ni uwezo wa betri kwenye simu husika. Realme 2 Pro inaelezwa kuwa na betri lenye 3500mAh ingawa haina teknolojia ya kuchaji haraka. Kuhusu programu endeshi ni Android 8.1.

INAYOHUSIANA  Matangazo Ya Samsung Kuwa Vifaa Vya Kuchajia Galaxy S10!

Bei+Rangi.

Realme 2 Pro inaelezwa kuuzwa kwa $192|Tsh. 441,600 yenye 4GB RAM/64GB memori ya ndani, $220|Tsh. 506,000 kwa yenye 6GB RAM/64GB diski uhifadhi na $250|Tsh. 575,000 ambayo ina 8GB RAM/128GB memori ya ndani.

Realme 2 Pro

Rangi tofauti tozauti za Realme 2 Pro.

Upatikanaji wake unategemewa kuwa mwezi Oktoba katikati na bei zote zilizoainishwa ni za ughaibuni.

Vyanzo: GSMArena, India Today

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.