Simu mpya ya Google iliyozinduliwa hivi karibuni imeingia dosari baada ya kugundulika kuwa na shida katika kioo chake, simu hiyo ya Pixel 2 XL ambayo imezinduliwa mwezi huu mwanzoni ilipata kupigiwa chapuo na mitandao mingi iliyoichunguza.
Imegundulika kwamba kioo cha Pixel 2 XL kimekuwa kinaacha alama za picha zilizopita, yaani ingawa umeshafungua picha ama kurasa nyingine kioo hicho bado kinakuwa na chembechembe ama mabaki ya picha au kurasa iliyopita.
Tatizo hili la kioo kwa kingeleza linajulika kama screen burn-in na halina madhara makubwa kwa utendaji wa kazi wa simu hii ila ni jambo la aibu kwa Google kuuza simu mamilioni ya pesa kisha simu hiyo ikawa na tatizo hata kama ni dogo.

Hata hivyo tatizo hili limeripotiwa kwa simu hiyo ya Pixel 2 XL pekee na sio kwa simu pacha ya Pixel 2 ambayo ni ndogo na pia inatumia kioo cha OLED kilichotengenezwa na Samsung wakati Pixel 2 XL yenyewe inatumia kioo cha OLED ila kilichotengenezwa na LG.
Ingawa ubovu huu wa kioo hauwezi kufananishwa na tukio la simu za Samsung kulipuka betri lakini ni wazi kwamba kampuni ya Google imepata pigo kubwa kwa sababu shida hii ya kioo itaharibu uhusiano wa kampuni hiyo na wateja wa vifaa vyake ambavyo ndio kwanza wameanza kutengeneza. Tazama picha mnato kujua zaidi.