fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Android LG simu Teknolojia

Simu janja za LG kupata masasisho ya Android 11, 12 na 13

Simu janja za LG kupata masasisho ya Android 11, 12 na 13

Mpaka sasa dunia nzima inajua kuwa LG itaachana na biashara ya simu janja mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu. Mbali na hilo ni wazi kuwa LG ina wateja wengi sehemu nyingi duniani na ni vyema wakafahamu kuwa simu janja zao zipo kwenye mpango wa kupata masasisho ya Android 11, 12 na 13.

Hivi karibuni LG walitangaza tarehe rasmi ambayo itajiweka pembeni kabisa na biashara ya simu janja lakini wakaweka wazi kuwa watamaliza kabisa rununu walizonazo ndani vilevile kuendelea kutoa masasisho ya programu tumishi kwenye simu zao ingawa itaakuwa ni kwa kipindi fulani tu.

SOMA PIA  .Com Imetimiza Miaka 30: Fahamu Historia Fupi

Sasa kwa mujibu wa tovuti za kampuni kwenye nchi za Ujerumani na Korea Kusini wameweka wazi kuwa baadhi ya simu zao zitapokea masasisho ya Android 11, 12 na 13. Hii maana yake ni nini? Hapa wana maana ya kuwa hata mara baada ya kufunga biashara ya simu janja mnamo Julai 31 wateja wenye rununu mbalimbali watapata masasisho ya Android 11, 12 mpaka 13.

kupata masasisho

Simu janja mbalimbali za LG zilizopo kwenye mpango wa kupokea masasisho ya Android 11, 12 na 13.

Simu ambazo tayari zimeshapokea/zitapokea masasisho masasisho ya Android 11

Tayari kupitia tovuti za LG nchini Ujerumani na Korea Kusini wameshaweka wazi orodha ya rununu ambazo zimeshapokea au zitapata masasisho ya Android 11 kama inavyoonekana pichani.

kupata

Orodha kamili ya simu janja za ambazo zimeshapokea Android 11 au zitapokea miezi michache ijayo.

kupata

Orodha inayoonyesha mwezi na mwaka ambapo simu husika imepokea/ipo kwenye mpango wa kupata masasisho ya Android 11. Q3=Robo ya tatu ya mwaka. Q4=Robo ya nne ya mwaka.

Vipi kuhusu Android 12 na 13?

Kwenye mpango huo wa LG imeweka wazi kuwa wateja wao pia watapokea masasisho ya Android 12 na 13. Hivyo, wateja wenye simu hizi hamna budi kutabasamu.

kupata

Hizo ndio rununu za LG ambazo zitapokea masasisho ya Android 12 na 13.

LG ndio hao mdogo mdogo wanawaaga wateja wao kwa kutoa habari njema kwao na sisi TeknoKona tumeshaleta mbele yenu taarifa hii. Daima tunasema msiache kutufuatilia.

Vyanzo: Android Authority, Gadgets 360, WCCF Tech

SOMA PIA  Teknolojia: Simu Janja na Apps Zinawasaidia Watu Wenye Matatizo ya Kuona (Vipofu)
Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania