fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

simu Tecno Teknolojia

Simu janja Tecno Spark 8 yazinduliwa huko Nigeria

Simu janja Tecno Spark 8 yazinduliwa huko Nigeria

Spread the love

Familia ya simu janja ya Tecno imeendelea kukua baada ya mwanafamilia mpya kuzinduliwa huko Nigeria. Tukiongelea simu janja za Tecno Spark hivi sasa imefikia toleo la 8.

Simu janja za Tecno Spark kwa mwaka huu pekee zimeshazinduliwa takribani 3 ikiwemo na hii ya sasa ambayo imezinduliwa huko Nigeria. Simu hii ipo katika mwonekano wa kisasa lakini unaovutia ambapo betri ya kwenye rununu hii ni kubwa. Sifa nyingine za kuhusu simu hii zinaridhisha kwani zinaendana na menggi ambayo soko la sasa linahitaji. Uchambuzi wake ni kama ifuatavyo:-

SOMA PIA  Kijana mmoja anasa kwenye choo akijaribu kuokoa simu janja

Muonekano|Kamera

Tecno Spark 8 ina kioo cha ubora wa IPS LCD chenye urefu wa inchi 6.5 na kama kawaida kamera ya mbele ya MP 8 imepambwa na sehemu iliyoingia ndani kidogo. Kamera kuu ina MP 16, ile ya mbili haijafahamika ni mahususi kwa ajili ya AI+taa ya kuongeza mwanga sehemu hafifu.

Spark 8

Tecno Spark 8 yazinduliwa na mfuniko wa nyuma ni wa plastiki.

Kipuri mama|Uwezo wa betri

Simu hii imewekwa kipuri mama MediaTek Helio P22 amabcho ni chenye nguvu zaidi kulinganisha na kile ambacho kipo kwenye Spark 7 (Helio A25). Kwa upande wa betri lina 5000mAh; inachaji kwa 10W kwa kutumia MicroUSB. Hapa zimepunguzwa 1000mAh kulinganisha na mtangulizi wake halikadhalika haina teknolojia ya kuchaji haraka.

SOMA PIA  Hii ni Simu janja Yenye Uwezo wa Kukaa na Chaji kwa Zaidi ya Siku 10

Memori|Mengineyo

Simu janja husika ina RAM GB 2 (GB 3 RAM-Spark 7), diski uhifadhi 64 GB lakini ikiwa na uwezo wa kuweka memori ya ziada. Simu hii inatumia HiOS 7.6, Android 11 Go Edition (tofauti na Android 11). Haitumia USB-C wala teknolojia ya kuchaji bila kutumia waya.

Spark 8

Muonekano wa nyuma halikadhalika teknolojia ya alama ya kidole.

Simu hii tayari imeshaanza kuuzwa huko Nigeria kwa karibu $130|zaidi ya Tsh. 299,000 lakini kimsingi ina mengi ambayo haina ukilinganisha na mtangulizi wake.

Vyanzo: GSMArena, Dignited

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania