fbpx
Anga, Ndege, Teknolojia

Angani kwa siku tano kwenye ndege ya abiria

siku-tano-angani-bila-kutua

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Ulishawahi kufikiria safari ya siku tano angani bila kubadilisha ndege? Sasa basi tumefika kwenye ulimwengu wa usafiri wa anga ambao hutahitaji kuunganisha ndege ili kufika unapokwenda.

Mamlaka ya usafiri wa anga ya Uingereza – CAA imetoa kibali kwa kampuni ijulikanayo kama Hybrid Air Vehicles (HAV) yenye makao yake katika mji wa Bedford kutengeneza ndege kubwa zenye uwezo wa kusafiri kwa muda mrefu (siku tano) bila ya kutua ardhini.

INAYOHUSIANA  Alama 'Kidole Chini' a.k.a 'Dislike' Haitakuja Facebook ~ Zuckerberg

Kampuni inayotaka kuunda ndege ndefu zaidi duniani imepewa kibali na sasa iko mbioni kuunda ndege hiyo ianze kubeba abiria. Hatua hiyo inafuatia kufanikiwa kwa majaribio ya ndege ya mfano iliyopewa jina Airlander 10 ambapo mwaka 2016 ndege moja ilidondoka baada ya kuruka kwa dakika 30 ilipokuwa kwenye majarbio.

siku tano
Sifa ya Airlander itakuwa na uwezo wa kukaa angani kwa siku tano bila ya kuhitaji mafuta,  lakini haitakuwa na kasi kubwa kama ndege nyingine.

Licha ya kubeba abiria vilevile itakuwa na uwezo wa kubeba mizigo tani 50, jambo ambalo ni gumu kwa ndege za kawaida.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: , ,

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.