fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Samsung simu Teknolojia

Sifa za simu janja Samsung Galaxy A22 5G

Sifa za simu janja Samsung Galaxy A22 5G

Spread the love

Ulimwengu wa sasa unaenda kasi kwa teknolojia ya 5G halikadhalika makampuni mbalimbali yamekuwa yakitoa simu janja ambazo zinakubali hapo tulipofikia hadi sasa na moja ya rununu hizo ni simu janja Samsung Galaxy A22 5G.

Mwezi Juni wakati simu janja Samsung Galaxy A22 4G inazinduliwa toleo la 5G lilitambulishwa pia ambapo rununu hizi zinafanana kwa mengi tuu mbali na muonekano wake lakini hata sifa zake za ndani zinazidiana kwa kiasi fulani ila kiujumla inaweza kuwa ngumu kidogo kuzitofautisha kwa macho. Hizi ndio sifa za simu janja Samsung Galaxy A22 5G:

Memori :
 • Diski uhifadhi: 64GB/128GB+sehemu ya kuweka memori ya ziada
 • RAM: GB 4/6/8
Betri/Chaji :
 • Li-Ion 5000 mAh
 • USB-C 2.0, OTG+uwezo wa kuchaji haraka kwa nguvu ya 15W
  Galaxy A22 5G

  Simu hii ina teknolojia ya 5G, redio ipo. Teknolojia ya kutumia alama ya kidole imewekwa kwa pembeni(kwenye kitufe cha kuzima/kuwasha simu), inatumia Bluetooth 5.0, WiFi. Uso wa mbele unalindwa na kioo kigumu na upande wa nyuma ni plastiki.

   

Kipuri mama :
 • MediaTek Dimensity 700 5G
Uzito :
 • Gramu 203

Programu Endeshi

 • One UI 3.1, Android 11
Rangi :
 • Nyeupe, Kahawia, Udhurungi
  Galaxy A22 5G

  Simu hii ipo katika toleo mbili tofauti; kuna moja inatumia kadi moja ya simu na nyingine ina uwezo wa kuweka laini mbili. Ina sehemu ya kuchomeka spika zxa masikioni, kipengele cha NFC kipo.

   

Simu hii inagharimu $230|zaidi ya Tsh. 529,000 (4/64), $255|zaidi ya Tsh. 586,500 (6/128) na $265|zaidi ya Tsh. 609,500 (8/128) kwa bei za ughaibuni na tayari ipo sokoni. Kumbuka kufuatilia TeknoKona ili uweze kuhabarika halikadhalika kuelimika kuhusu teknolojia.

Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania