fbpx
Kompyuta, TCRA, TEHAMA, Teknolojia

TCRA kuwashindanisha vijana wa vyuoni katika shindano la udukuzi

shindano-la-udukuzi-na-ulindaji-taarifa-mtandaoni
Sambaza

TCRA kupitia kitengo chao cha ulinzi wa kompyuta wa dharura, TZ-CERT imeleta shindano kwa wanavyuo wachukuao masomo ya teknolojia ambalo litawafanya wanafunzi kuweza kudukua taarifa na kujilinda na mashumbulizi kupitia shindano la kudukua (HACKING COMPETITION).

Shindano hilo lipo kwa ushirikiano na kampuni ya Silensec litawajumuisha wanafunzi wote wa vyuo vya Tanzania watakaojisajili kupitia tovuti yao ya cyberstars. Tanzania inakua nchi ya pili ya Afrika Mashariki baada ya Rwanda kujiunga katika shindano hilo. Shindano la udukuzi

picha : cyberstars

Shindano la udukuzi linalenga wanafunzi wa vyuo wenye uri kati ya miaka 18-24 wanaosoma masomo ya Sayansi ingawa hata wale ambao hawasomi masomo hayo lakini wanapenda kufahamu namna ya kulinda taarifa wanaruhusiwa kujiunga kwenye shindano hilo.

Shindano la udukuzi
Tanzania yajiunga kwenye shindano la udukuzi.

Hii ni nafasi kubwa kwa wanafunzi na watu wengine kuonyesha ujuzi wao katika nyanja hii ya udukuzi ambao kwa hili tunaita udukuzi wa faida kiasi kwamba kama utaonyesha uwezo wako mkubwa wa kudukua na kujilinda na mashambulizi basi utakuwa umejiongezea nafasi kubwa ya kutambulika kitaifa na kufikisha ndoto zako kuwa za kweli.

Shindano hili ni muhimu hasa kwa wanafunzi kwani linaongeza ujuzi kuzingatia wataalamu wa usalama wa kompyuta tanzania ni mdogo sana hivyo kama wewe ni mwanafunzi basi tembelea kwenye tovuti yao ya CyberStar halafu fanya usajili subiri maelekezo ambapo washindani watapewa makabrasha ya kusoma kwa muda wa miezi 6 kabla ya shindano kuanza.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Watafiti: Factory Reset katika Simu za Android Haifuti Data Zako Zote
0 Comments
Share
Tags: ,

Lymo

A Cyber Security Guy | A student | I Know A lot