fbpx

Uganda: Sheria ya kodi ya mitandao ya kijamii kupitiwa upya

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Serikali ya Uganda imetangaza kwamba sheria mpya ya tozo ya kodi kwenye mitandao ya kijamii itaangaliwa upya kufuatia maandamano yaliyofanyika nchini humo.

Hata hivyo, hakuna uhakika kuwa kodi hiyo itaondolewa kabisa au huenda ikachukua wiki kadhaa kabla ya kuidhinishwa mabadiliko yoyote yale.

Serikali ya Uganda ilipitisha sheria ambayo ilianza kutumika Julai Mosi ambayo inatoza kodi ya shilingi za Uganda 200 kila siku kwa anayetaka kutumia mitandao ya kijamii.

INAYOHUSIANA  Nani Mtawala Katika App Za Ku Chati Kwa Sasa?

Tamko la serikali limekuja baada ya siku ya Jumatano kufanyika maandamano makubwa ya wananchi kupinga kuwepo kwa kodi hiyo inayomuumiza mwananchi.

Maandamano hayo yaliongozwa na mbunge na mwanamuziki nchini Uganda Robert Kyagulany, maarufu kama Bobi Wine ambapo polisi walijaribu kumkamata lakini alifanikiwa kutoroka.

Sheria ya kodi ya mitandao ya kijamii: Maandamano yaliyofanyika nchini Uganda kupinga kodi ya kwenye mitandao ya kijamii. Kampeni hiyo inafahamika kama #ThisTaxMustGo.

Polisi walilazimika kurusha mabomu ya gesi ya kutoa machozi na kufyatua risasi hewani ili kutawanya kundi la waandamanaji wanaopinga kodi iliyoidhinishwa ya kutumia mitandao ya kijamii.

Wabunge wengi wametaka sheria hiyo ifutwe au isimamishwe kwa muda kupisha mjadala mpana kuhusiana na sheria hiyo yanayotarajiwa kuanza Alhamisi ya wiki ijayo.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.