fbpx

Taasisi ya Sayansi China yakuza mpunga mpya wenye urefu wa mita 2.2

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Baada ya utafiti uliodumu kwa miaka 10, taasisi ya Sayansi ya kilimo nchini Uchina imeweza kukuza mpunga wa aina mpya ambao una urefu wa kufikia mita 2.2.

Kwa mujibu wa taasisi ya kisayansi ya Institute of Subtropical Agriculture (ISA) imesema mpunga huo mpya utazalisha mchele mwingi tofauti na mpunga ulizoeleka. Kwa kawaida mpunga wa kawaida huwa na urefu wa mita 0.9 hadi mita moja.

Taasisi ya Sayansi China yakuza mpunga mpya wenye urefu wa mita 2.2

Taasisi ya Sayansi China yakuza mpunga mpya wenye urefu wa mita 2.2: Shamba maalum lenye uwezo wa kutoa mpunga wenye urefu wa mita 2.2.

Shamba maalum lilitengwa kwa ajili ya ufaiti huo lilikuwa katika mji wa kaunti ya Changsha, katika jimbo la Hunan nchini Uchina. Mtafiti wa idara hiyo Bw. Xia Xinjie amesema kuwa mpunga huo unafanya usanisinuru kwa ufanisi mkubwa zaidi kuliko mpunga wa kawaida kwa asilimia 50.

INAYOHUSIANA  Nubia Red Magic 3 kuzinduliwa Aprili 28

Kwa wastani mmea mmoja una machaka 40, mpunga unaokua kwenye chaka moja unaweza kufikia zaidi ya 500, na uzalishaji wa michele unaweza kufikia tani 12 kwa hekta.

Mpunga huo una shina nene lenye kipenyo cha milimita 18.5, na majani yake yanafunikwa na nta, hivyo ni vigumu kuangushwa na upepo, unakinga wadudu na mafuriko.

Bw. Xia amesema mpunga huo umekuwa wenyewe kwa kutumia teknolojia mbalimbali mpya zikiwemo kuchochea mabadiliko ya mpunga, kukuza mpunga chotara kwa kutumia mpunga pori, na kuchagua aina nzuri za mpunga kwa mujibu wa alama za molekuli.

Mkurugenzi wa idara hiyo Bw. Wu Jinshui amesema mpunga huo mrefu unapandwa kwenye mashamba yenye maji ya kina, hivyo utaweka mazingira mazuri kwa ufugaji wa samaki mashambani.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.