fbpx
Samsung, Teknolojia, Uchambuzi

Samsung yaweka rekodi kwa kupata faida ya mamilioni ya dola ndani ya siku moja

samsung-yaweka-rekodi-kwa-kupata-faida-ya-mamilioni-ya-dola-ndani-ya-siku-moja

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Samsung ambayo mwaka 2016 haukuwa mwaka mzuri kwao kutokanana kupata misusuko ya aina mbalimbali na kupelekea kampuni hiyo kuyumba kwa namna fulani baada ya kupata kashfa za simu yake ya Note 7 kulipuka  🙄 🙄 lakini sasa mambo yamezidi kuwaendea sawa.

Kuna biashara ambayo haikudhaniwa kama ingewafanya Samsung kuendelea kupata faida ya juu mbali na biashara yao iliyozoeleka ya simu janja lakini sasa biashara hiyo inaonekana kuwa nuru kwa Samsung kutokana na bidhaa hizo kuhitajika na makampuni mbalimbali na biashara hiyo ni ya utengenezaji wa chip.

Mchanganuo wa faida waliyoipata Samsung kutokana na mauzo ya prosesa (chip) wanazozitengeneza.

Katika kipindi kama hiki mwaka uliopita (2016) Samsung iliweza kupata kiasi cha faida halisi baada ya kukatwa kodi ya 148% (kwenye masuala ya uchumi na fedha kitu kupata zaidi ya 100% inawezekana). Mwaka 2017 katika kipindi chha mwezi Julai-Septemba Samsung imweza kupata faida ya $10.6bn.

INAYOHUSIANA  Samsung wazindua Galaxy A11 kimyakimya

Samsung imekuwa ikifanya vyema sana kwa uppande utengenezaji wa prosesa ambbazo makampuni mbalimbali akiwemo Apple kuomba kutengenezewa memory chips za kutumia kwenye bidhaa zake. Samsung inatarajiwa kuendelea kufanya vizuri zaidi kutokana na prosesa zinazotengenezwa na Samsung kuhitajika kwa wingi.

Moja ya chips zilizotengenezwa na Samsung. Biashara ya prosesa inafanya Samsung kuweza kufanya vizuri baada ya kupata majanga ya kwenye Note 7.

Hata kama Samsung imeweka rekodi lakini wapo wanaoamini kuwa mafanikio yanayooenekana hivi sasa kwa Samsung ni matunda ya juhudi za uwekezaji wa huko nyuma. Utakumbuka kuwa aliyekuwa mkurugenzi wa Samsung alishtakiwa na kupelekea kampuni hiyo kupata doa kutokana na kiongozi wa juu wa kampuni hiyo kushtakiwa.

INAYOHUSIANA  Simu Mpya Za Firefox Kuja Afrika

Samsung imeweka nguvu sana kwenye simu zenye kamera mbili za nyuma, teknolojia ya AI ambayo ipo kwenye simu, utengenezaji wa sensors za 3D bila kusahau utengenezaji wa prosesa ambao unaonekana kushamiri na mahitaji yake kuongezeka.

Chanzo: The guardian

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|