Katika intaneti yenye kasi hivi sasa katika nchi zetu za Afrika ni teknolojia ya 4G na hiki ndio kizazi kinachoonekana kuwa chenye kasi ya intaneti lakini hali ni tofauti kwa Samsung ambao wanafikiria kuhusu kizazi cha 5 cha intaneti.
Tangu mwaka 2015 Samsung imeunganisha nguvu na kampuni nyingine ya mawasiliano ya Japani inayofahamika kama KDDI katika kufanikisha teknolojia ya intaneti ya 5G inatumika kwenye bidhaa/huduma kati ya makampuni hayo mawili.
Samsung kwa kushirikiana na KDDI ilifanya majaribio ya kasi ya intaneti ya 5G kwenye treni ya mwendokasi na kasi ya intaneti hiyo ikiwa ni 1.7Gbps.
Kilichofanyika kwenye majaribio ya intaneti ya 5G.
Kwenye majaribio hayo ambayo yalifanyika kwenye treni iliyokuwa ikisafiri kwa kasi ya zaidi ya Km 100/saa ilihusisha kifaa cha kisasa zaidi cha kuongeza kasi ya intaneti kama ikiwa ndogo (5G router), 5G Virtualised Radio Access Unit (vRAN) na Virtualised core.
Treni hiyo ambayo ilikuwa kwenye kasi huku umbali kati ya vituo viwili ukiwa karibu Km 1.5; ilishuhudiwa katika majaribio hayo video ya kiwango cha 8K kupakuliwa pamoja na video ya kiwango cha 4K iliyokuwa inachukuliwa ndani ya treni kutoka kwenye kamera iliyokuwa eneo la mbele ndani ya treni kuweza kuwekwa (uploaded).
Usalama wa teknolojia hiyo umearifiwa kuwa ni wa kuaminika kwa maana ya uduukuzi (udukuzi wa WI-FI, wizi wa taarifa za abiria, n.k) na kuwa yenye kasi zaidi itakayowafurahisha abiria/watumiaji wa teknolojia hiyo.
Tangu mwaka 2015 Samsung na KDDI wamekuwa wakifanyia majaribio teknojia ya 5G. KDDI wenyewe wanatarajia kuanza kutumia teknolojia ya intaneti ya 5G mwaka 2020.
Matumizi ya teknolojia ya 5G yanatarajia kufungua milango kwa aina mbalimbali za biashara kufikiria kutoa huduma hiyo huku KDDI wakiahidi kuendelea kufanyia majaribio teknolojia hiyo katika sekta mbalimbali.
Vyanzo: Gadgets 360, ZDNet