Mwaka 2022, Samsung ilitazamiwa kuzindua mwendelezo wa toleo la simu janja kutoka kwenye familia ya “S” kwa maana ya Galaxy S22 FE lakini suala hilo limewekwa kando na maana yake simu hiyo haitatoka tena mwaka huu.
Katika miaka ya karibuni makampuni mengi ambayo yanafanya shuguhli za kutengenza na kuuza simu janja ama vifaa mbalimbali vya kidijiti zimejikuta zikilazimika kuhairisha kutoa bidhaa fualni kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao. Vivyo hivyo, kwa upande wa Samsung wamejikuta wakiachana na mpango wa kuzindua Galaxy S22 FE mwaka huu kutokana na sababu kadha wa kadha.
Mosi, Samsung imehairisha mpango wa kuzindua Galaxy S22 FE kutokana na changamoto ya upatikanaji wa kipuri mama cha kutumika kwenye kifaa husika ambapo janga la virusi vya Corona liliathiri kwa kiasi kikubwa utengenezaji wa vipuri, bidhaa mbalimbali duniani kote.
Pili, wakati upamde mmoja ilikuwa ikipambana na uhaba wa upatikanaji wa vipuri mama kwa ajili ya kutumika kwenye Galaxy S22 FE upande wa pili mahitaji ya simu janja Samsung Galaxy S22 Ultra yaliongezeka sokoni hivyo kuifanya kampuni kuweka nguvu kubwa kwenye bidhaa ambayo soko inaihitaji zaidi kwa wakati huo. Hivyo, ikafika hatua ya kuchagua ama Galaxy S22 FE au Galaxy S22 Ultra.

Mipango ya mbeleni
Samsung wanajipanga kutengeneza simu janja takribani milioni 3 ambazo ni za toleo la Fan Edition (FE) na mpango huo ukilenga Galaxy S23 FE. Kwa sasa Samsung inapambana kuhakikisha inauza Galaxy S22 Ultra takribani milioni 10 hadi mwisho wa mwaka huu pekee na mapema mwakani inapanga kuongeza mauzo ya rununu husika kwa 30% hivyo kufikia simu janja milioni 13 za Galaxy S22 zilizouzwa. Mauzo ya Galaxy S23 yanatazamiwa kufikia rununu 8.5 milioni ambazo zimeuzwa na S23 Plus ikitazamiwa kuleta mauzo ya chini kabisa-6.5 milioni.
Kwa makadirio hayo, unaiona Samsung kwenye nafasi gani ya ushindani wa kimauzo kwenye robo ya mwisho kwa mwaka 2022? Tunakaribisha maoni yako.
Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.