fbpx
Samsung, simu, Teknolojia

Samsung polepole wanatoka kwenye kioo chenye duara katikati

samsung-polepole-wanatoka-kwenye-kioo-chenye-duara-katikati
Sambaza

Simu nyingi katika miaka ya karibuni zimekuwa zikiwekewa nakshi nakshi kwa sehemu inapokuwa kamera ya mbele kuachwa uwazi mithili ya herufi “V” au kuwa na duara dogo kuzunguka eneo hilo la kamera ya mbele.

Samsung wanaonekana kutaka kuja na kioo ambacho kitakuwa hakina duara dogo kwenye eneo la kamera ya mbele na pengine kuweza kufikria kuwa simu hiyo itakuwa haina uwezo wa kupiga zile picha za kujipiga mwenyewe lakini kumbe ni katika hali tu ya kutaka kuja na kitu ambacho kitakuwa cha kitfauti zaidi sokoni mathalani Samsung Galaxy A90 simu ambayo inatazamiwa kutoka mwanzoni mwa mwezi Aprili 2019.

INAYOHUSIANA  Microsoft kwenye iPhone: Word, Excel, na Powerpoint kuwa kwenye app moja

Je, kamera ya mbele kwenye Samsung Galaxy A90 itakuwa wapi?

Kwa haraka haraka unaweza ukafikiri simu hiyo huenda kamera ya mbele haipo kabisa la hasha! Ila ukiwa mpekuzi utaweza kutambua kuwa imefichwa kidogo na itambidi mtu kupandisha kidogo eneo la juu upande wa kushoto kuweza kuiona ilip na hata kuitumia kisha kuirudisha mahali pake.

kioo chenye duara
Samsung Galaxy A90-Mpangilio wa kamera kwenye simu husika.

Teknolojia hiyo unaweza ukaifananisha kiasi na Samsung Galaxy S8/S9 ambazo haina dura dogo lakini kamera ya mbele inaonekana dhahiri kwa juu. Mwisho wa yote tusubiri Aprili 10 kuweza kuona iwapo Samsung watazindua Samsung Galaxy A90 simu pekee kutoka kwao kutokuwa na kioo chenye duara dogo katikati.

Vyanzo: CNET, GSMArena

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|