Ni mara chache sana kuona kampuni fulani imetumia imeweka kioo kisichovunjika kwenye toleo fulaani au hata kubaki kuwa ni mipango tu ambayo mara nyingine isikamilike kwa wakati na kubaki kuwa ni habari tu.
Mara baada ya majaribio kadhaa mpaka kujiridhisha Samsung imethibitisha kuwa teknolojia yao ya kutumia ya kioo (display) aina ya OLED chenye sifa moja kuu ya kutovunjika imepitishwa.
Kioo hicho kilipitishwa karika vikwazo mbalimbali na kuweza kuhimili (kutopata athari yoyote/kuvunjika). Majaribio hayo yalikuwa ni:-
kudondoshwa mara 26 kutoka juu mpaka chini kwa umbali wa karibu futi 4 (mita 1.2), kuwekwa sehemu yenye joto la juu lililofikia nyuzi joto 71 (159.8°F) na katika wango cha chini cha joto kilichofikia -31°C (-25.6°F) bila kupata athari zozte zile.

Vioo ya namna hiyo vinaelezwa kuweza kutumika katika vitu mbalimbali mfano kwenye TV za magari, vifaa vya kucheza magemu, vifaa vya kijeshi, tabti, n.k lakini Samsung hawajaweka wazi ni lini wataanza kutumia teknolojia hiyo.
Vyanzo: The Verge, Engadget