fbpx

Samsung kuongeza ubora wa kamera

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Makampuni mbalimbali duniani ambayo yanajishuguhlisha na biashara ya simu janja katika moja ya vipengele ambavyo wanahakikisha vitawavutia watu mara moja ni kwenye ubora wa kamera.

Samsung wameonyesha nia ya kufanya bidhaa zao zijazo kuwa na nguvu zzaidi upande wa kamera baada ya kuzindua vipuri viwili tofauti ambavyo vitafanya kamera za kwenye simu janja ziwe na MP 32 na MP 48; vipuri hivyo ni ISOCELL Bright GM1-MP 48 na ISOCELL Bright GD1-MP 32.

ubora wa kamera

Vipuri ambavyo vinatazamia kuwekwa kwenye simu janja zijazo kutoka Samsung.

Kwanini iwe vipuri hivyo?

Katika teknolojia ya kisasa zaidi makampuni mengi yanaonekana kutumia vitu vyembamba sana, vidogo lakini vyenye uwezo mkubwa ndani yake ambapo kwa vipuri vinavyotazamiwa kutumika kwenye matoleo yajayo upande wa simu janja na hssa kwenye kamera.

Teknolojia iliyopo nyuma ya pazia (ISOCELL) ina uwezo wa kuunganisha vipande vinne vya ubora wa picha (pixels) na kupata kitu kimoja/picha ambayo ni bora zaidi.

ubora wa kamera

Utofauti ubora wa kamera kwenye simu janja mbalimbali.

Samsung wanatazamiwa kufanya mabadiliko kwenye simu zao kwa kuboresha kamera kuanzia mwakani (2019). Vipi kitu hicho kitakufanya uzidi kupenda rununu za Samsung?

Vyanzo: GSMArena, Mr. Phone

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Samsung Fold kuchelewa kuingia sokoni: Samsung wabadilisha tarehe
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.