Pengine hii inaweza kuwa ndio simu janja ya kwanza (kutoka Samsung?) ambayo ina betri la kutoka kuwa na uwezo mkubwa kuliko zote.
Fununu za jina ni kwamba inaitwa Galaxy Xcover 6 Pro, na kwa sasa kuna mpaka picha ambazo zinasambaa katika mtandao zikiwa zinaonesha simu hiyo.

Hatujaona simu janja ambazo zina betri ya kutoka moja kwa moja kwa kipindi cha muda mrefu sana, pengie Samsung ndio wanakuja kubadilisha jambo hili.

Simu hii itatambulishwa rasmi mwezi julai 2022 na pengine hapo ndipo tutakapoweza kujua sifa zake za undani kabisa, lakini kwa haraka haraka inabidi tusahau tuu uwezo wa kuzuia kuigia na maji.

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, hivi ni simu janja gani ya mwisho wewe kutumia ?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.