Simu hizi za kujikunja zina umaarufu sana kwa sasa lakini cha kushangaza bado watu wengi hawajaweza kujaribu simu hizi, Samsung imeeleza baadhi ya mipango yao kuhusiana na simu hizi.
Kwa mwaka huu kampuni ya Samsung ina mpango wa kuuza simu za kujikunja (Foldable) ambazo zinafika milioni 10.

Kumbuka kwa sasa simu za kujikunja zinazotegemewa sana kutoka ni katika kampuni ya Samsung ni Galaxy Z Fold 4 na Galaxy Z Flip 4 ambazo zote ni za kujikunja.
Na kama inavyojulikana simu janja za aina hii huwa hazina soko kubwa sana ukilinganisha na simu janja za kawaida.

Mpango mwingine kutoka kwa kampuni hiyo ni kwamba mpaka kufikia mwaka 2025 wanataka mauzo ya simu za kujikunja yafikie angalau nusu ya mauzo ya simu janja za kawaida.
Samsung wamesema kuwa bei za simu janja za kujikunja kutoka kwako zimeshushwa sana ili kuhakikisha zinawafikia watu wengi Zaidi licha ya kuwa na gharama kubwa katika uzalishaji.
Lakini kwa baadhi ya wadau wanasema kuwa ni simu janja ambazo zina bei za juu na kitu cha ajabu zaidi ni simu ambazo ni rahisi sana kuharibika na hata kuchukua ukubwa Zaidi katika mfuko wako.
unakumbuka ile kesi ya simu ya kwanza ya kujikunja kutoka Samsung ambayo ilileta shida kipindi cha mwanzo kabisa katika sokoni? isome zaidi >>HAPA<<
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie katika eneo la comment, je hii umeiopokeaje, na wewe unaweza kuanza kutumia simu janja za mfumo huu?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.