fbpx
Android, Android Pie, simu, Teknolojia

Samsung Galaxy S9/S9+ yapokea Android Pie

samsung-galaxy-s9-s9-yapokea-android-pie
Sambaza

Samsung ambao walitoa Samsung Galaxy S9 na S9 Plus mwezi Februari 2018 huku ikiwa na Android 8 lakini sasa hatimae sasa watu wanaomiliki simu hizo wameanza kupokea taarifa fupi ya kuweza kuhamia Android Pie.

Kwa hakika ambao wanatumia Sammsung Galaxy S9/S9+ wamesubiri kwa miezi kadhaa tangu kutoka kwa toleo la kenda upande programu endeshi kwa simu za Android.

Kwa taarifa zilizopo wanaotumia simu tajwa huko Ujerumani, Uholanzi. Italia, Uswizi wameweza kupata taarifa fupi kuhusu kuweza kupakua masasisho ya Android 9.

Android Pie
Mchakato wa kuhamia kwenye Android kutoka tole lililopita.

Kama imeanza kwa watumiaji wa simu husika kutoka nchi nyingine basi sio vibaya na sisi wengine tukaanza kuangalia upande wa settings>>about phone>>software update ili kuweza kujua kama Android Pie imesharuhusiwa kuja.

Vyanzo: Android Police, GSMArena, Tech Radar

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Miaka 30 ya mafaili ya mtindo wa GIF. - Fahamu historia yake!
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|