fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Samsung simu Uchambuzi

Samsung Galaxy S21, S21 Plus na S21 Ultra – Simu mpya za Kisasa kwa mwaka 2021 kutoka Samsung

Samsung Galaxy S21, S21 Plus na S21 Ultra – Simu mpya za Kisasa kwa mwaka 2021 kutoka Samsung

Spread the love

Kwa kufungua mwaka 2021 Samsung waleta simu mpya za kuvutia zinazobeba majina ya Sumsang Galaxy S21, S21 Plus na S21 Ultra.

Samsung Galaxy S21 inaanza kupatikana kwa bei ya dola 799, takribani Tsh 1,860,000/= wakati Galaxy S21 Plus inaenda kwa bei ya dola 999 ambayo ni takribani Tsh 2,330,000/= . Simu zote zitaanza kupatikana kuanzia Januari 29.

SIMU ZA Samsung galaxy s21 na s21 plus

Simu hizi mbili zinafana kwa kila kitu kwa ndani tofauti kubwa ikiwa ni ukubwa. Galaxy S21 ikiwa na ukubwa wa inchi 6.2, huku Galaxy 21 Plus ikiwa na ukubwa wa kioo wa inchi 6.7.

Sifa za Galaxy S21 na S21 Plus

galaxy s21 na s21 plus

Display/ Kioo cha teknolojia ya Dyanamic AMOLED, 120 Hz kikiwa na pixels 1080 kwa 2400 kikilindwa na teknolojia ya Corning Gorilla Glass Victus.

SOMA PIA  Motorola wametoa nyingine inaitwa Moto Z3

OS: Zinakuja na Android 11

Chip – Toleo la Marekani na China linakuja na Qualcomm SM8350 Snapdragon 888 wakati toleo la kimataifa litatumia chip za Samsung za Exynos 2100 (5nm)

Disk na RAM – Kutakuwa na matoleo ya GB 128 na 256, lakini yote yatakuja na RAM ya GB 8.

Kamera Kuu – Inakuja na kamera tatu,

  • Ya megapixel 12 inayojikita kwenye kupiga picha pana.
  • Ya megapixel 64 kwa ajili ya kupiga picha za umbali, ina uwezo wa zoom ya kawaida/optical ya mara 1.1 huku hybrid zoom (digital+optical zoom) ya uwezo wa mara 3
  • Ya megapixel 12 kwa ajili ya upana mkubwa zaidi pamoja na uwezo wa kuchukua picha za video
SOMA PIA  Umoja wa Ulaya kudhibiti gharama za simu

Kwenye video inaweza kupiga picha za ubora wa 8K@24fps, 4K@30/60fps, 1080p@30/60/240fps, 720p@960fps, HDR10+, stereo sound rec., gyro-EIS

Kamera ya Selfi
Inakuja na uwezo wa megapixel 10, Auto HDR na uwezo wa kuchukua video za ubora wa 4K@30/60fps, 1080p@30fps

Mawasiliano: Nje ya teknolojia tulizozizoea simu hii inakuja na uwezo wa teknolojia ya mawasiliano ya kisasa ya 5G

Betri na kuchaji: Galaxy S21 inakuja na betri la mAh 4000 huku Galaxy S21 Plus ikija na betri la mAh 4800

Kwenye kuchaji simu zote zinakuja na uwezo wa kuchaji bila kutumia waya /wireless charging. Pia zinakuja na port za USB Type C zenye uwezo wa kuchaji kwa haraka (25W).

SOMA PIA  Uhai wa tafiti za kisayansi nchini Uingereza

Vingine:
Fingerprint, Redio za mfumo wa sterio, hakuna port ya headphone/audio jack.

galaxy s21

Nje ya Samsung Galaxy S21 na S21 Plus, Samsung wametambulisha pia simu ya Galaxy S21 Ultra. Simu iliyokubwa zaidi kiumbo, yenye kamera nyingi zaidi pamoja na uwezo wa kutumia kalamu/stylus.

Kikubwa katika matokeo haya simu tunaanza kuona kushuka kwa bei za simu za hadhi ya juu. Ukilinganisha na matoleo ya nyuma ambayo yanapewa sifa ya ‘flagship premium’, yaani matoleo ya simu za hadhi ya juu yanayobeba kampuni kwa mwaka jana wastani wa bei ilikuwa ni kuanzia dola 1000 za Kimarekani ila kupitia Galaxy S21 tunaona Samsung kaanza na dola 799.

Ni kawaida kwenye sekta ya simu bei kushuka na kupanda kutokana na ujio teknolojia mpya zinazosababisha gharama mpya katika utengenezaji na vipuri.

Tutegemee kuona maendeleo makubwa katika upatikanaji wa simu za 5G kwa bei nafuu kwa mwaka huu.

Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania