fbpx
Samsung, simu, Teknolojia

Samsung Galaxy S10 haitakuwa na 5G

samsung-galaxy-s10-haitakuwa-na-5g
Sambaza

Dunia ya leo inaendelea kusonga mbele kila kukicha na baada ya teknoloja ya 4G katika suala zima la kufanya mawasiliano na matumizi ya intaneti, 5G ipo mlangoni tayari kupata nafasi yake.

Soko linatarajia kuona kuwa baadhi ya chapa maarufu zilizopo sasa zikiboreshwa kwa kuwekewa teknolojia ya 5G walau katika nusu ya kwanza ya mwaka 2019. Samsung Galaxy S10 ni mojawapo ya toleo maarufu linalotarajiwa kuwekewa mfumo wa 5G wakati itakapotoka.

Hata hivyo, kampuni ya Samsung imethibitisha kwamba toleo lake la kwanza la simu ya mfumo wa 5G  haitakuwa Galaxy S10. Kampuni hiyo ya Korea Kusini imepanga kuzindua simu za 5G ifikapo mwezi Machi 2019.

Galaxy S10
Samsung wameweka wazi kuwa teknolojia hiyo ya 5G itakuwepo kwenye simu rununu nyingine kutoka kwao lakini sio Samsung Galaxy S10.

Kwa sasa hakutakuwa na mabadiliko katika uzinduzi wa simu kutoka familia ya “S” katika nusu ya kwanza na muendelezo wa “Note” katika nusu ya pili ya mwaka.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Fahamu Kuhusu Kipimo cha HIV Kinachotumia Simu Janja
0 Comments
Share

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.