fbpx
Samsung, Teknolojia

Samsung Galaxy Fold: Simu inayojikunja Kioo Kuuzwa Rasmi Aprili 26

samsung-galaxy-fold-kuuzwa-rasmi-aprili-26
Sambaza

Imepita miezi miwili sasa tangu kampuni pendwa ya simu za mkononi ya Samsung kuitambulisha simu yao yenye muonekano tofauti kabisa katika soko la simu. Sasa imeshafahamika ni lini simu hiyo itaingia sokoni.

Rununu, Samsung Galaxy F ni simu inayojikunja imekuwa ikiongolewa na watu wengi sana na imekuwa chini ya kampuni yao tu kwa muda wote na kutoruhusu mtu yeyote kuigusa. Kuanzia jana tarehe 15/04/2019 wahusika waliweza kuruhusu watu mbali na wachambuzi wa simu kuzigusa na kupiga picha.

INAYOHUSIANA  Samsung kufungua kiwanda kikubwa India
Simu inayojikunja
Samsung Galaxy F au simu inayojikunja.

Simu hii itaanza kupatikana na kuuzwa rasmi kuanzia tarehe 26 mwezi huu wa nne. hivyo kama wewe ni mpenzi mzuri wa simu mpya za kisasa basi kuanzia tarehe iyo unaweza pitia katika stoo zao za SAMSUNG.

Simu inayojikunja

Simu hiyo yenye thamani ya $1,980 sawa na pesa ya kitanzania shilingi 4,587,264. Je, wewe ni mpenzi wa simu za Samsung? Basi jiandae kuweza kuinunua kuanzia Aprili 26.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Lymo

A Cyber Security Guy | A student | I Know A lot