fbpx
Samsung, simu, Teknolojia

Samsung Galaxy A50 yapata masasisho ya usalama

samsung-galaxy-a50-yapata-masasisho-ya-usalama
Sambaza

Kila siku tunatumia simu janja zetu lakini si wengi ambao huwa tunafikiria kupakakua masasisho ya usalama ili kufanya simu janja zetu kwenye sehemu nzuri za kutodukuliwa jambo ambalo linasabsbisha madhara kwa namna moja au nyingine.

Uimara wa simu janja tunazotumia unatokana na mambo mbalimbali na moja ya vitu hivyo ni kuhakikisha kifaa chako kinapakua masasisho, hii itasaidia kwenye kuepusha matatizo ya kidukuzi na kiutendaji kwenye simu yako.

INAYOHUSIANA  Ijue OnHub, Router Mpya Kutoka Google!

Baada ya kusema hayo nikwambie tuu Samsung Galaxy A50 imeruhusiwa kupokea masasisho kwa dhumuni la kwenda kurekebisha na kuboresha mambo kadhaa katika utendaji wake.

Mapema mwezi Juni 2019 Samsung walitoa sasisho ambalo lililenga kufanya maboresho kwenye upande wa kamera-kipengele cha “Slow Mo” lakini pia kuongezwa kwa muonekano wa giza. Safari hii masasisho ya usalama yanaleta njia fupi ya kuweza kutumia QR scanner lakini pia maboresho kwenye kamera na WiFi.

INAYOHUSIANA  Google Goals; Njia ya kufikia malengo yako kwa kalenda janja
masasisho ya usalama
Masasisho ya usalama kwenye Samsung Galaxy A50.

Usisahau kuwa na kifurushi cha intaneti zaidi ya MB 190 ili kuweza kushusha faili husika. Sasi huwa tunawajali kila leo basi usisite kutupa maoni yako/kuuliza maswali.

Vyanzo: Gadgets 360, GSMArena

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|