fbpx

Samsung Fold kuchelewa kuingia sokoni: Samsung wabadilisha tarehe

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Samsung Fold kuchelewa kuingia sokoni kuliko ilivyopangwa mwanzoni, Samsung watoa tamko rasmi baada ya ubovu wa display ulioonekana baada ya waandishi wa habari kadhaa kupatiwa kwa uchambuzi wa siku chache.

samsung galaxy fold Samsung Fold kuchelewa

Simu ya Samsung Fold

Siku chache zilizopita tuliripoti kuhusu skendo ya aina yake iliyotokea kwenye simu mpya za Samsung Fold baada ya waandishi wa habari na wachambuzi kadhaa kupewa simu hiyo kwa matumizi ya siku chache. Simu hii itakayokuwa na bei juu ya milioni 4.5 za Kitanzania ilionekana ikiharibika display ndani ya utumiaji wa chini ya siku 3.

INAYOHUSIANA  Simu mpya za iPhone kwa mwaka 2018

Tazama video hapa:

Samsung walikuwa wamelenga simu hiyo inanze kupatikana ramsi tarehe 26 mwezi huu kwa Marekani, na kisha kuanza kupatikana pia kwenye masoko mengine duniani kote.

Katika taarifa yao Samsung hawajasema rasmi tarehe ya upatikanaji wa simu hiyo tena, ila wamesema wamesogeza mbele wakitumia muda kufanyia maboresho matatizo yaliyojitokeza. Pia wataweka maelekezo mazuri ya jinsi ya kutumia simu hiyo kwani kuna baadhi ya matatizo yaliyojitokeza yanayoonekana kusababishwa na utumiaji mbovu kwa waliopewa simu hiyo hapo mwanzo.

samsung fold zaharibika

Uharibifu wa display katika Samsung Fold

Kuna hatari sana kutumia bidhaa zinazokuja na teknolojia mpya, ila ni hatari zaidi kama mtumiaji atatoa zaidi ya milioni 4 kununua bidhaa itakayoharibika baada ya siku kadhaa, inaonekana Samsung wamechukulia suala kwa mapana zaidi na hivyo kuona bora kuchelewa kuliko kuleta bidhaa itakayoleta shida kwa maelfu ya watumiaji.

INAYOHUSIANA  Samsung kuongeza ubora wa kamera

Je una mtazamo gani kuhusu simu hii? Soma uchambuzi wetu hapa -> Hii ndio Samsung Fold.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.