Je unafahamu ya kwamba Samsung walikuwa wameshikilia rekodi ya utengenezaji wa diski ya SSD yenye ujazo mkubwa zaidi?
Rekodi hiyo waliiweka takribani miaka miwili iliyopita walipotambulisha diski ya SSD yenye ujazo wa TB 15.36 – kwa wakati huo ndio ilikuwa kubwa zaidi.

Diski yao mpya ina ujazo wa TB 30.72 na ina ukubwa wa inchi 2.5 tuu. Katika utendaji kazi pia toleo hili ni bora zaidi, uhamishaji wa mafaili (copying/transfer) ni karibia mara mbili zaidi ukilinganisha na toleo la TB 15.36 – kasi ya usomaji na uhamishaji mafaili wa MB 1,700 hadi MB 2,100 kwa sekunde.
Pia inategemewa kutokana na mafanikio yao waliyoyapata katika utengenezaji wa diski hizi Samsung watatumia teknolojia hiyo kutoa tena matoleo ya ujazo mdogo kwa bei nafuu pia kuliko zamani.
Je unafahamu tofauti ya diski za SSD na HDD? Soma makala yetu -> Tofauti ya SSD na HDD.
Chanzo: Engadget na tovuti mbalimbali