fbpx
Anga, Ndege, Usafiri, Usalama

Sababu 5 kwanini ndege inapata ajali

sababu-5-kwanini-ndege-inapata-ajali
Sambaza

Habari yoyote ya ajali ya ndege inawasababisha watu wengi wawe na wasiwasi kuhusu usalama wa ndege, na kushuku kama kuna mashambulizi ya kigaidi au la!

Lakini ukweli ni kwamba kuna sababu mbalimbali zinazopelekea ndege kupata ajali. Tumeona tuziangazie sababu tano zinazosababisha ajali ya ndege kutokea:

1. Makosa ya rubani

Siku hizi ndege zina sifa nzuri zaidi na zinaaminika zaidi, hivyo makosa ya rubani yamesababisha ajali nyingi za ndege, ambazo zinachukua asilimia 50 ya ajali zote. Ndege ni chombo chenye utatanishi mkubwa. Rubani wanapoendesha ndege kwa hatua mbalimbali, ni rahisi kufanya makosa.

INAYOHUSIANA  Waiba Tsh Bilioni 27.9 katika zaidi ya ATM 1,400 ndani ya masaa 3!

2. Matatizo ya vifaa au teknolojia kwenye ndege

Ingawa ndege zinasanifiwa na kutengenezwa vizuri zaidi siku hadi siku, lakini asilimia 20 ya ajali za ndege bado zinasababishwa na matatizo ya vifaa kwenye ndege. Injini ikishindwa kufanya kazi, ajali zitatokea.

Ndege nyingi za siku hizi zinakuja na teknolojia kubwa ya kujiendesha yenyewe – na hivyo kumpunguzia mzigo rubani. Ila sifa kubwa ya programu za kompyuta ni uwezekano wa makosa ya kiprogramu kutokea, na kumbuka programu hizi zinahusisha uwezo wa hadi kuielekeza ndege ishuke kiasi au kupanda juu kiasi kulingana na data ambazo programu inazisoma wakati wa safari husika. Mfano ajali ya ndege ya Ethiopian Airline – wachambuzi wa masuala ya ndege wanawasi wasi mkubwa itakuwa imehusisha makosa katika teknolojia ya namna hii.

INAYOHUSIANA  Boeing wasimamisha utengenezaji wa ndege za 737 Max

Kwanini ndege

3. Hali mbaya ya hewa

Asilimia 10 ya ajali za ndege zinasababishwa na hali mbaya ya hewa. Ingawa vifaa vingi vipya vya elektroniki vimewekwa kwenye ndege, vikiwemo gurudumu tuzi, GPS na mfumo wa data za hali ya hewa, lakini ndege bado ni dhaifu zikikabiliwa na dhoruba, theluji kubwa na ukungu.

4. Vitendo vya kuharibu ndege kwa makusudi

Asilimia 10 ya ajali za ndege zinasababishwa na vitendo vya kuharibu ndege kwa makusudi. Lakini ni kweli njama hizi zimesababisha ajali nyingi na hasara kubwa.

INAYOHUSIANA  Kaspersky yakiri kupakua nyaraka za siri za Marekani

5. Makosa ya kibinadamu

Sababu nyingine ya ajali ya ndege kutokea ni makosa ya kibinadamu. Kila kitu kinaweza kuwa sawa katika ndege kuanzia hali ya hewa mpaka mawasiliano. Lakini kutokana na udhaifu wa kibinadamu ajali huweza kutokea. Makosa ya kibinadamu yamesababisha ajali za ndege kwa asilimia 7.

Ajali ni kitu ambacho unaweza ukaepukana nacho na kuwa slama kabisa hivyo daima tuwe katika tahadhari tunapokuwa katika vyombo vya moto.

~ Masasisho (updates) madogo yamefanyika tarehe 12-03-2019

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.