fbpx
Roboti, Teknolojia

Roboti ya kupiga kinanda yaundwa Uingereza

roboti-ya-kupiga-kinanda-yaundwa
Sambaza

Wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Cambridge nchini Uingereza wametengeneza mkono wa roboti wenye uwezo wa kupiga kinanda.

Mkono huo wa bandia, uliotengenezwa kwa kutumia mbinu ya printer 3D, unaweza kucheza nyimbo za muziki kwenye kinanda kwa kusogeza mkono.

kinanda
Ni suala la muda tuu mbadala wa binadamu kutumika kupiga ala za muziki utapatikana.

Wakifafanua kuwa ni vigumu sana kutengeneza harakati za mkono na vidole kama alivyo binadamu, wataalamu hao wamefanikiwa kuiga mkono wa binadamu ambao unaweza kucheza nyimbo rahisi ikiwemo ya Jingle Bells na baadhi ya nyimbo zingine ilizofundishwa.

INAYOHUSIANA  Samsung: Majaribio ya kioo kisichovunjika yafaulu
kinanda
Utafiti huo utawezesha kutengeneza roboti wenye uwezo wa kufanya harakati kama binadamu kwa kutumia nishati ndogo katika kupiga kifaa hicho.

Hata hivyo, wanasayansi hao wamesema sio rahisi kwa sasa roboti hiyo kupiga kwa ufasaha kila nyimbo isipokuwa wanaendelea kufanya utafiti kuwezesha hilo.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: ,

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.