fbpx
simu, Teknolojia

Robo ya kwanza mwaka 2020 kwa mauzo ya simu

robo-ya-kwanza-mwaka-2020-kwa-mauzo-ya-simu
Sambaza

Mwaka 2020 umekuwa na mengi lakini kubwa zaidi ni kuhusu virusi vya Corona ambavyo vimeyumbisha uchumi wa Dunia kwa asilimia kubwa tuu; kuhusu kiasi gani cha simu zimefika sokoni simu huko ni huzuni!.

Makampuni yanayotengeneza simu janja na kufanikisha kuzisambaza nchi mbalimbali duniani ndio kitu kinachokuja kuzalisha “Mauzo kwenye robo ya kwanza, pili, tatu”. Sasa kutokana na janja la homa kali ya mapafu inayosababisha na virusi vya COVID-19 makampuni mengi kama si yote yamekumbnana na changamoto ya kufikisha bidhaa zao sokoni.

INAYOHUSIANA  Obama atajua juu ya John Snow kabla yetu.

Hata hivyo, Xiaomi na Realme zimeonekana kupanda kimauzo (kama inavyoonekana pichani) mbali na kwamba kampuni nyingi zimeyumba kimapato.

Mauzo ya simu
Usafirishaji wa rununu kwenye robo ya kwanza mwaka 2020: Mamilioni ya rununu/asimilia ya mauzo katika kipindi sawa na hicho mwaka 2019.

Wataalamu wa kuchambua wa takwimu za mauzo ya simu wanasema kwenye robo ya mbili mwaka huu bado athari ya janga la virusi vya Corona itaendelea kuonekana kwani kuna makampuni yatakuwa yanapambana kujiweka sawa kibiashara hatimae kuongeza faida.

Kiujumla usafirishaji wa simu janja umeshuka kwa 13% ambapo mara ya mwisho hali hiyo kutokea ilikuwa ni mwaka 2014. Samsung, Huawei na Apple ndio zipo tatu bora. Je, kwenye robo ya pili mambo yatakuaje? Tusubiri kuweza kufahamu na TeknoKona tutakubahabarisha.

Vyanzo: GSMArena, Counterpoint

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|