fbpx

Robo ya kwanza 2018: Nokia yashika nafasi ya 5 kwa mauzo soko la Ulaya

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Simu za Nokia zimechangia kuuza kwa asilimia 3.5 katika soko la Ulaya katika robo ya kwanza ya mwaka 2018 na kupelekea kushika nafasi ya tano kwa uuzaji wa simu nyingi.

Kulingana na uchambuzi na utafiti wa kampuni ya Canalys Nokia imeuza simu milioni 1.6 na kufanikiwa kusafirisha simu milioni 6.3.

Sambamba na hilo simu za kampuni ya Samsung na Apple licha ya kuendelea kuongoza kwa mauzo lakini takwimu zinaonesha mauzo yake yameshuka katika robo ya kwanza barani Ulaya.

Robo ya kwanza 2018

Samsung ambao bado wanaongoza kwa kuuza zaidi lakini mauzo yake yameshuka kwa asilimia 15.4 wakati simu za iPhone zimeshuka mauzo yake kwa asilimia 5.4.

Utafiti unaonesha bado simu za Nokia zinapendwa lakini kupotea katika soko kwa muda kumewafanya wapenzi wao kuhamia kwenye simu za aina nyingine.

Nokia imeshauriwa kuendelea kutoa matoleo mazuri yenye ushindani katika soko la simu za kisasa ili kuweza kushika soko.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Nubia Alpha: Simu janja inayovaliwa mkononi
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.