Ripoti: Yaliyosakwa zaidi na Wakenya mwaka 2017 mtandaoni

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Mwaka 2017 ndio huo upo ukingoni kumalizika na hatimae kuanza mwaka mwingine. Google imekuwa msaada kwa watu wengi duniani kwa kuwezesha kutoa majibu kwa mambo mbalimbali.

Ripoti iliyotolewa na kampuni ya Google inaonyesha uchaguzi wa Kenya pamoja na Tume huru ya Uchaguzi (IEBC) ndio vitu vilivyotafutwa zaidi nchini Kenya kwa mwaka 2017. Mbali na hayo rais wa zamani wa Kenya, Mwai Kibaki ni miongoni mwa watu waliotafutwa zaidi kwenye Google.

jinsi ya kupika chapati, kupata mimba, namna ya kupunguza kitambi, kupunguza mafuta mwilini, maradhi kipindupindu na maradhi ya kupooza ya Guillain–Barré syndrome (GBS) ni miongoni mwa masuala yaliyotafutwa (search) zaidi mtandaoni na Wakenya kwa mwaka 2017.

Kulingana na Mkurugenzi wa Uhusiano Mwema wa Google, huenda wengi wa waliosaka jinsi ya kupata mimba ni wasichana na wanawake. Google imekiri kuwa hawajui jinsi ya kupata mimba bali labda walikuwa wakitafuta namna ya kujizuia.

Ugonjwa wa GBS unasababisha misuli kuwa dhaifu hivyo kufanya mwathiriwa kupooza. Mambo mengine yaliyotafutwa zaidi mtandaoni ni jinsi ya kupata matokeo ya mtihani wa Darasa la Nane (KCPE) mtandaoni na kuandika wasifu kazi (CV).

Orodha ya mambo mbalimbali yaliyotafutwa zaidi na Wakenya kwa mwaka 2017.

>Watu maarufu

 • Mwai Kibaki
 • Babu Owino
 • Ezra Chiloba
 • Janet Kanini
 • Nicholas Biwott
 • Robert Mugabe
 • Joseph Nkaissery
 • Nderitu Gachagua
 • Jimmy Wanjigi
 • Chris Msando

 

>Matukio maarufu

 • Mgomo wa walimu wa elimu ya juu
 • Pigano la ngumi kati ya Mayweather na McGregor
 • Kombe la shirikisho
 • Kombe la mataifa ya Afrika 2017
 • Zimbabwe coup
 • Hurricane Irma
 • Pasaka 2017
 • Uhuru wa Catalonia
 • Ramadan 2017

 

>Wanamichezo

 • Alvaro Morata
 • Romelu Lukaku
 • Philippe Coutinho
 • Nemanja Matić
 • Ivan Perisic
 • Thomas Lemar
 • Cheick Tiote
 • Antonio Conte
 • Dennis Oliech
 • Floyd Mayweather

 

>Burudani

 • Despacito
 • Odi dance
 • Bazokizo
 • Zilipendwa
 • Shape Of You
 • Nyashinski Malaika
 • Big Brother Naija
 • Bet Awards 2017
 • Eunice Njeri Wedding
 • Beyonce Twins

Kila mwisho mwa mwaka Google hutoa ripoti ya namna watu walivyosaka mambo kadhaa kwa wingi zaidi kwa kila nchi na dunia kwa ujumla.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Kumbukumbu ya miaka 25 kwa tovuti ya kwanza duniani kuwa hewani (Online)
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.