fbpx

Rihanna ajizolea karibu dola 1bn kutoka kwa Snapchat

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Utajiri unaweza kutokana na sababu mbalimbali na sasa mwanamziki wa miondoko ya RnB amejiongezea utajiri wake baada ya kulipwa karibu $1bn na Snapchat Inc. kutokana na kejeli!

Mzaha mzaha hutumbua usaha” ni msemo ambao una maana kubwa katika kila jambo ambalo unaweza ukafikiri lisiwe na madhara makubwa lakini mwisho wa siku ukaishia kuingia gharama ambazo hukuzitarajia.

INAYOHUSIANA  Messenger Lite; App ya kuchati ya Facebook kwa simu za uwezo mdogo

Rihanna ameshika vyombo vya habari duniani baada ya kuilalamikia Snapchat kwa kumtumia yeye pamoja na Chris Brown katika matangazo ya kwenye mtandao wa kijamii wa Snapchat; tangazo hilo liliuliza iwapo mtu “Angechagua kumchapa kibao Rihanna au kumpiga ngumi Chris Brown“.

Rihanna ajizolea karibu dola 1bn kutoka kwa Snapchat

Tangazo la Snapchat lasababisha Rihanna kulipwa karibu dola bil. 1 za kimarekani.

Msanii huyo wa RnB aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba tayari Snapchat wanajua kuwa huo sio mtandao wa kijamii anaoupenda na angeweza kulinyamazia jambo hilo la kejeli lakini ameamua kufanya hivyo kuwawakilisha wanawake, wanaume pamoja na wale wote ambao ameshawahi kutumiwa na makampuni mbalimbali kuwakejeli.

Rihanna ajizolea karibu dola 1bn kutoka kwa Snapchat

Ujumbe mkali kutoka kwa Rihanna kwenda kwa Snapchat baada ya kumkejeli kwenye tangazo la Snapchat lililomlenga yeye (Rihanna) na Chris Brown.

Snapchat waliomba msamaha kwa Rihanna na kudai kuwa tangazo hilo lilitoka kimakosa bila ya kupitiwa lakini mameno hayo hayakumshawishi msanii huyo kuweza kuisamehe kampuni hiyo na kuacha jambo hilo lipite tu.

Vyanzo: Telegraph, Today Fm

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|