fbpx
Gemu

Rekodi Iliyowekwa Na Pokemon Go!

rekodi-iliyowekwa-na-pokemon-go

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Pokemon Go tangia iachiwe rasmi mwezi wa saba mwanzoni 2016 imeleta mafanikio makubwa sana. Mpaka sasa imeshashushwa zaidi ya mara milioni 30

Kingine cha aina yake ni kwamba mchezo huu umechukua muda wa siku saba tuu kuweza kushushwa mara milioni 10. Yaani wiki moja mchezo huu umeshushwa mara milioni 10 na ni rekodi ya aina yake ambayo yaijawahi kuwekwa na gemu yeyote ya simu

INAYOHUSIANA  Seagate waanza Kuuza Diski ya TB 8


Pokemon Go imeweka rekodi hii kwa kuizidi Clash Royale siku mbili zaidi na kuizidi siku tano Candy Crush Jelly Saga

Ripoti hizi zinametolewa na kampuni ya utafiti ya SensorTower na moja kati ya masoko makubwa ya mchezo huu ni huko Japan

Ukiachana na mchezo kama mchezo bado Pokemon Go imeleta faraja kubwa sana katika kampuni la Nintendo. Hisa za Nintendo zimeongezeka thamani katika bei zake kupitia mchezo huu

INAYOHUSIANA  Mcheza Gemu Aishtaki Bethesda Kwa Kuifanya ‘Fallout 4’ Imtawale Mpaka Apoteze Kazi Yake!

Lakini hata hivyo sio wao tuu ambao wanapata asali kupitia mchezo huo wa Pokemon, baadhi ya wataalam wametabiri kuwa kampuni ya Apple inaweza ikaingiza mapato ya dola bilioni 3 kati ya miezi 12 mpaka 24 ijayo kupitia mchezo huo.

Apple wanapokea asilimia 30 ya mauzo katika mchezo huo na watabiri wengi wanasema kuwa manunuzi mengi (80%) ya gemu hiyo yanafanyika kwa kutumia vifaa vya iOs

INAYOHUSIANA  Sony Waamua Kusitisha 'Playstation Mobile'
Gemu ya Pokemon Go
Gemu ya Pokemon Go

SOMA PIA: Pokemon Go: Gemu Tishio Kwa Mitandao Ya Kijamii

Hii inaonyesha ni jinsi gani kitu kidogo kinavyoweza kuingiza pesa kama kikitengenezewa mazingira.

Wakati Pokemon Go inaweka rekodi na sisi TeknoKona tunazidi kukuachia rekodi ya kuwa namba moja Tanzania kwa habari zote za kiteknolojia

Niandikie sehemu ya comment hii umeipokeaje, ningependa kusikia kutoka kwako. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
1 Comments
Share
Tags:

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

1 Comments

  1. Gemu ya Pokemon Go yafanyiwa maboresho ya aina yake - TeknoKona
    February 16, 2017 at 10:33 am

    […] gemu hili linaingia sokoni lilitokea kupendwa sana na kuongeza soko la Nintendo mara mbili zaidi kwa kiasi cha dola za Kimarekani 43 milioni ( zaidi ya Tsh. 94.2 bn) imefanyiwa […]