fbpx
Magari, Usafiri

Rais Kagame azindua gari la kwanza lililounganishwa Rwanda

rais-kagame-azindua-gari-la-kwanza
Sambaza

Rais Paul Kagame wa Rwanda amezindua gari la kwanza aina ya Volkswagen lililounganishwa kwenye kiwanda cha Volkswagen kilichopo Kigali-Rwanda.

Gari hilo aina ya Polo ni la kwanza kuunganishwa katika kiwanda hicho huku kampuni hiyo ya magari ya Ujerumani ikitarajiwa kuunganisha vipuri vya magari 5,000 katika  awamu ya kwanza ambayo kati yake yatakuwa ni magari aina ya Passat, Tiguan, Amarok na Teramont.

INAYOHUSIANA  Uganda: Mabasi ya umeme Jua kuanza kutengenzwa kwa wingi
Rais Kagame azindua gari
Rais Kagame akiwa katika uzinduzi wa gari aina ya VW lililounganishwa nchini kwake.

Kampuni ya magari ya Volkswagen ambayo ndio kubwa zaidi barani Ulaya, imefanya uwekezaji wa $20m (£15m) nchini Rwanda na ikitarajiwa kuajiri watu 1,000.

Kampuni hiyo inapanga kuuza magari hayo mbali na kuyatumia kama usafiri wa kukodi (taxi) ambapo wateja watawasilisha maombi ya kutaka huduma hiyo kupitia simu zao.

Rais Kagame azindua gari
Uunganishwaji wa magari ukiendelea

Kuna takribani magari 200,000 ya watu binafsi yaliosajiliwa katika taifa hilo lenye zaidi ya watu milioni 12 kulingana na halmashauri ya kutoza ushuru nchini humo. Kampuni hiyo ya Ujerumani inapanga kupanua uwekezaji wake katika eneo la jangwa la Sahara baada ya kufungua kiwanda chake nchini Kenya 2016.

INAYOHUSIANA  Serikali ya Uchina na magari yanayotumia umeme
Rais Kagame azindua gari
rais kagame akiendesha gari lililotengenezwa Rwanda

Wengine hawaamini kwamba magari ya Ujerumani yanaweza kuunganishwa nchini Rwanda, na leo tayari magari ya kwanza yamezinduliwa. Kiwanda hiki ni mwamko mpya katika safari ya Rwanda ya ukuwaji wa kiuchumi~Paul Kagame

Hata hivyo, $15,000 ambalo ndio gari (VW) la thamani ya chini zaidi; ni wazi kwamba magari hayo yatakuwa ghali mno kwa raia wengi nchini Rwanda.

Volkswagen tayari imejikita katika baadhi ya nchi barani Afrika, ambazo ni pamoja na Nigeria, Afrika Kusini na Kenya.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.