fbpx
Android, apps, Google Pay, Teknolojia

Playstore ya muonekano mpya kwa wote

playstore-ya-muonekano-mpya-kwa-wote
Sambaza

Tunaponunua simu janja ni lazima kuwa na akaunti ya Gmail kitu ambacho ni kitambulisho chako kwenye Google Playstore ili kuweza kupakua programu tumishi mbalimbali. Sasa je, unafahamu kuwa soko hilo lina muonekano mpya kwa wote?

Simu za Android zipo nyingi tuu sokoni na hata mikononi mwa watu (wanaozitumia) katika kufanikisha mawasiliano ya kila siku kwenye dunia iliyotawaliwa na utandawazi kwa sasa. Mbali na hilo baadhi ya wenye rununu hizo zenye toleo la Android 10 wamekuwa wakiweza kubadilisha muonekano wa Playstore kutoka mng’avu kwenda kwenye giza na wamekuwa wakifurahia hilo kwa mizezi kadhaa sasa.

INAYOHUSIANA  Google kushirikiana na Fiat Chrysler katika Uletaji wa Magari Yajiendeshayo Yenyewe

Google wameona inafaa kwa wenye simu janja za Android zinazotumia toleo la chini ya  Android 10 nao pia kuweza kupata muonekano mpya kwa wote  wanapotembelea soko hilo kwa matumizi mbalimbali. Si jambo gumu (linalochukua muda) kuhama na kuingia “Gizani”; ni suala la kuingia kwenye mpangilio ndani ya Playstore kisha theme na kuhamisha kutoka kwenye light kwenda dark.

muonekano mpya kwa wote
Muonekano wa giza kwa simu za Android.

Kuwa huru kwa kujifunza mengi kupitia usomaji wa makala zetu na uwe mwalimu kwa wengine. Haya kama wewe unatumia simu ya Android na hukua unafahamu kuhusu hili basi kabadilishe muonekano kama utapenda. Usisite kutupa maoni yako lakini pia kutufuatilia kila leo.

Vyanzo: GSMArena, Life Hacker

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|