Sambaza
WhatsApp kupitia tovuti yake imetangaza kwa watumiaji wa programu hiyo pendwa, kwamba sasa imewezesha watumiaji hao kuweza kupiga simu kwa njia ya WhatsApp (video/sauti peke yake) kwa watu wanne kwa wakati mmoja.
Ujio wa kipengele hicho ulitangazwa tangu mwezi Mei mwaka huu katika mkutano wa Facebook F8. Mtumiaji wa WhatsApp ataingia katika WhatsApp yake na kumpigia simu ya video/sauti peke yake rafiki yake kisha kwa upande wa kulia juu ataona alama ya kitufe cha kumuongeza (add participant) mtu mwingine.

Idadi ya kuongeza watu itakuwa mwisho ni wanne na wote kutaweza kuzungumza kwa njia ya WhatsApp. Kipengele hiki kitasaidia kuendesha mijadala kwa watu watakaopenda kufanya hivyo.
Ili uweze kupata kipengele hicho utalazimika ku tumia toleo la WhatsApp lenye sasisho hilo/utumie WhatsApp Tester ili uwe wa kwanza kupokea masasisho.
Ikiwa hutakipata kipengele hicho licha ya kuifanyia masasisho WhatsApp yako, basi utalazimika kusubiri mpaka maboresho hayo yatakapokufikia.
Facebook Comments
Sambaza