fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Teknolojia

Pata kuifahamu simu janja Tecno Pova 2

Pata kuifahamu simu janja Tecno Pova 2

Spread the love

Mwaka huu wa 2021 mpaka sasa tayari kuna simu janja nyingi tuu sokoni zilizotengenezwa na Tecno na siku si nyingi zilizopita ilizinduliwa Tecno Pova 2.

Kila mara ambpo simu janja ya Tecno inatoka ikiwa imelengawatumiaji wa uwezo wa juu/kati huwa navutiwa kutaka kujua undani wa rununu husika. Tecno Pova 2 ni simu janja yenye mengi mazuri hasa kwa wanaopenda magemu. Sifa zake ni kama ifuatavyo:-

SOMA PIA  Baada ya Kutumia Mabilioni, Jeshi la Marekani Lasita Utumiaji wa Roboti katika Ubebaji wa Mizigo

Kipuri mama|Ukubwa wa kioo

Raha ya kucheza gemu kwenye simu basi inapendeza iwapo rununu ina uwezo uliojitosheleza. Simu hii ina kioo chenye ung’avu wa hali ya juu sana (1080p+), kioo chake kina urefu wa inchi 6.9. Halikadhalika, kwa upande wa kipuri mama ni Helio G85 inayoelezwa kuwa na nguvu kiasi cha kufurahisha wakati wa kucheza magemu.

Uwezo wa Kamera|Memori

Idadi ya kamera kwenye simu hii ni tano nyuma na moja mbele. Upande wa nyuma unaongozwa na MP 48, MP 13 na tatu zina MP 2. Kamera ya mbele ina MP 8 huku RAM yake ni GB 6 kwa 128GB za diski uhifadhi lakini inawezekana pia kuweka memori ya ziada.

Tecno Pova 2

Tecno Pova 2 imelenga zaidi wanaopenda kucheza magemi kwenye simu janja.

Uwezo wa betri|Mengineyo

Hapa betri wameweka kubwa; 7000mAh halikadhalika teknolojia ya kuchaji haeaka kwa 18W, sehemu ya kuchomeka chaji ni USB-C. Ni simu janja ya 4G LTE, ina redio, Bluetooth 5.0, inatumia kadi mbili za simu.

SOMA PIA  Google wazindua Nearby Share

Bei ya simu hii ni $167|zaidi ya Tsh. 384,100 ambapo hiyo ni bei ya ughaibuni na itaigia sokoni kuanzia Julai 11 ya mwaka huu. Ile huduma ya kununua kabla ya kitu hakijaingia sokoni itaanza Juni 6.

Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania