Kwenye suala zima la ushindani wa biashara ya saa janja makampuni mengi yamekuwa yakifanya maboresho kila toleo moja baada ya jingine na siku si nyingi tutaweza kufahamu undani wa Oppo Watch 3.
Mbali na simu janja Oppo imeweka nguvu nyingi tuu kwenye saa janja ambazo zimekuwa zikitoka toleo moja hadi jingine mwaka hadi mwaka. Oppo ambao wamekuwa kampuni ya kwanza kutumia kipuri mama cha Snapdragon W5 kwenye Watch 3 ikiwa ni kifaa ambacho Qualcomm ilikitambulisha siku kadhaa zilizopita ikiwa ni mahususi kutumika kwenye saa janja.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Oppo zinasema ujio wa Oppo Watch 3 haitakuwa peke yake kwa maana ya kwamba zitaziduliwa zaidi ya saa janja moja kutoka familia moja. Na kiuhalisia matoleo ya juu maana yake yatakuwa na uwezo zaidi kwa maana ya kwamba hata kipuri mama kitakuwa chenye ubora zaidi ya hicho ambacho kimetumika kwenye toleo hilo jipya la saa janja kutoka Oppo.

Mbali na Oppo, inatazamiwa kuwa tutaweza kuona ujio wa saa janja nyingine ambayo hadi sasa jina rasmi la bidhaa hiyo bado halijawekwa wazi lakini wengi wakiamini kuwa itakuwa ni “TicWatch Pro 4” ambayo inatumia Snapdragon W5+ ikiwa ni kipuri mama cha pili kilichotengenezwa na Qualcomm mahususi kwa ajili ya saa janja lakini ni mojawapo kati ya vifaa viwili vilivyozinduliwa hivi karibuni.
Watu wengi wanaamini kuwa vipuri hivyo vitakuwa na ufanisi mzuri na kufanya saa hizo janja kuwa na betri ambalo linadumu na chaji kwa muda mrefu. Sisi yetu ni macho na kusubiri kuona iwapo zitatuvutia kuweza kuzinunua au tutaziacha zitupite.
Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.