iCloud Imejaa? Fanya Haya Kuongeza Ujazo!

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Tumepata malalamiko wengi kwa watumiaji wa iPhone na kikubwa ni kwenye iCloud za vifaa vyao kuwa zinajaa ndani ya kipindi cha muda mfupi. Kuna mambo mengi sana ambayo yanapelekea simu hizo kujaa katika ujazo-uhifadhi wa kimtandao wa iCloud.

Kwa kawaida Apple wanatoa GB 5 za bure katika iCloud hivyo zikijaa mtu ana uwezo wa kulipia kiasi cha pesa ili kupata ujazo zaidi na kuendelea kufurahia huduma hiyo. Hili lisipowezekana basi mtumiaji hana budi kufuta baadhii ya mafaili katika kifaa chake ili angalau awe una ujazo wa kutosha.

icloud apple

Huduma ya iCloud inahusisha hifadhi ya data mbalimbali muhimu za mtumiaji wa bidhaa za Apple; hii ni pamoja na picha, data za mafaili, contacts na data zingine mbalimbali

Wengi katika vifaa vya Apple wanajishau na kuruhusu mafaili mengi sana (picha, video, nyaraka n.k) kuingia moja kwa moja katika iCloud zao. Ni wazi kuwa icloud kwa kawaida inahifadhi mambo mengi sana ili kuifanya isijae inabidi kuzuia mambo mengi kuingia moja kwa moja katika ujazo uhifadhi huo, au kuruhusu mambo kidogo tuu kuingia.

INAYOHUSIANA  Samsung yaamriwa kuilipa Apple mabilioni!

Njia Za Kuongeza Ujazo Ni Kama Ifuatavyo

  • Usihifadhi (Back Up) Vitu Vingi Sana

Cha msingi kujua ni kwamba back  up ile ya moja kwa moja (automatic) kabisa ndio mara nyingi inachukua sehemu kubwa aya uhifadhi na hapo kuna aina mbili kuna uhifadhi wa ‘system’ nzima na kuna ule uhifadhi wa App moja moja mfano back up ya WhatsApp.

Hapo cha kufanya ni kuingia katika Settings > ingia katika jina lako > iCloud kisha nenda katika Storage. lakini hii inaweza ikawa inatofautiana kwa toleo na toleo, kwa mfano katika iOS 11 ni Manage Storage > Backups naiOS 10 ni iCloud Storage > Manage Storage. Ukishafika hapo basi unaweza futa hiyo back up na vile vile una uwezo wa kuzuia kabisa system kuweza kuji back up tena.

INAYOHUSIANA  Mambo nane binafsi ya kustaajabisha kuhusu Steve Jobs!

Kwa App moja moja ni rahisi sana unaweza ukaenda kutika iCloud serttings na ukaanza kuzuia au kufuta uwezo wa App moja moja kuweza kuji’back up

Muonekano Wa iCloud

  • Njia Zingine Mbadala
  • Fanya Kifaa Chako Kuwa Na Picha Chache

Ni wazi simu zetu siku hizi zina ujazo uhifadhi mwingi sana, hii inapelekea mara nyingi kupiga picha nyingi sana na mwisho wa siku tunachagua moja au mbili tuu ambazo tunakua ndio tumezipenda na zile zingine zote tunajisahau hatuzifuti.  Kwa kuzifuta picha ambazo hatuna mpango nazo itasaidia sisi kupata nafasi nyingi katika simu hivyo hata ukiamua kuziback up katika icloud zitaenda chache

  • Futa Meseji Zako Za Nyuma

Ndio hata meseji (kama unatumia na iMessege mara kwa mara ndio meseji zitakuwa na ukubwa zaidi)  huwa zinaenda kujiback up katika iCloud, kama utakua na tabaia ya kufuta zile za nyuma ambazo hazima maana tena basi katika simu yako kutakua na ujazo wa kukutosha na pia kama ukiamua kufanya back up katika iCloud bila shaka zitachukua ujazo mdogo tuu.

  • Futa Mafaili Katika iCloud Drive
INAYOHUSIANA  Biashara ya vioo kati ya LG na Apple

Usipokua makini unaweza ukashanga iCloud drive yako inajaa ni vitu kadha wa kadha ambavyo huvihitaji tena. Kwa mfano unaweza ukashanga kuna mafaili kibao kama vile video na documents (PDFs n.k) ambazo huna mpango nazo tena. Ni vyema kufuta mafaili haya ili kuweza kufurahia kifaa chako.

Mpaka hapo nadhani unaweza sasa ukafanya mwenyewe na ukafanikiwa kuongeza baadhi ya nafasi katika ujazo uhifadhi wa iCloud. Kama nilivyosema awali njia kuu ni moja tuu nayo ni kutoruhusu kifanyaa chako kufanya back up nyingi katika kifaa chako maana hizo ndizo zinazokuja kujaza nafasi katika iCloud. Njia nyingine zilizobaki ni kukusaidia tuu katika kuhakikisha simu yako ina nafasi ya uhifadhi wa kutosha

Ningependa kusikia kutoka kwako wewe hili unalionaje? ningeoenda kusikia kutoka kwako. Niandikie hapo chini katika sehemu ya maoni.

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.