Makampuni mengi yanajitahidi kuweka nguvu zaidi kwenye matumizi ya dijitali ambapo imeonekana kuwa inaokoa muda na mambo si hapa kwani sasa unaweza ukalipia bidhaa mtandaoni kupitia M-Pesa.
Vodacom kwa ushirikiano na MasterCard pamoja na benki ya BancABC watamuwezesha mtumiaji yeyote wa huduma ya M-Pesa kuweza kutengeneza kadi ya MasterCard kwa njia ya M-Pesa na muda huo huo kuweza kuhamishia pesa kwenda akaunti hiyo na kisha kuweza kuanza kuitumia mara moja kufanya manunuzi mtandaoni.
Hii ina maanisha;
- Hakuna haja ya wewe kwenda kufungua akaunti benki ili kuweza kupata kadi itakayokuwezesha kufanya malipo ya mtandao: kadi za Visa au MasterCard.
- MasterCard kupitia huduma ya M-Pesa wataweza kukupatia namba ya kadi yako ya njia ya kimtandao – ambapo namba za kadi hiyo utaweza kuzitumia kufanyia malipo ya mtandao bila wasiwasi wa kuibiwa kwenye akaunti yako ya M-Pesa kwani akaunti hii mpya ya MasterCard itakuwa inajitegemea.
Kwa kawaida huwa suala zima la kununua kitu kupitia tovuti fulani na kufanikiwa kufanya malipo ni jambo ambalo linahusisha benki yako kwa njia ya Visa au MasterCard au huduma ya PayPal lakini Vodacom Tanzania imefanikiwa kurahisisha mambo zaidi na hivyo kuweza kutumia salio lako kwenye M-Pesa kuweza kulipia bidhaa fulani kutoka mtandaoni na kisha kuipta baada ya muda fulani.
Utafanyaje/itakuaje kufanikisha malipo?
Jambo hili limewezeshwa kwa mtu mteja yeyote wa M-Pesa, kwa lugha rahisi ni kwamba hutahitaji kuwa na akaunti ya benki/namba ya kadi inayohusu kwenye benki fulani.
Utaingia kwenye menyu ya M-Pesa kama kawaida kwa kupiga *150*00# kisha utachagua namba 4 na baada ya hapo utabofya namba 6 halafu chagua namba 1. Utapokea ujumbe mfupi wa maneno ambao utakuwa na taaarifa muhimu utakazojaza kufanikisha malipo ya bidhaa unayotaka kununua. Picha jongefu ifuatayo inaeleza kwa kina:-
2 Comments
Comments are closed.