Sio mara nyingi kwa programu ambazo hazitengenezwi na kampuni kubwa kupakuliwa (Downloaded) na mamilioni ya watu wengi kabla ya kufikia ukomo na kupotea kabisa.
Lakini hili ni tofauti na App ya Nova Launcher ambayo imetengenezwa na Kevin Barry wa TeslaCoil Software mpaka sasa imepakuliwa na watu zaidi ya milioni 50 duniani kote. Nova Launcher kwa sasa ndio inayoonekana kupendwa na watu wengi zaidi kuliko nyingine yoyote. Inapatikana Play Sore kwa Simu Janja za Android.
Aidha kuweka toleo la Beta na kusikiliza kile watumiaji wanachotaka ndani ya Nova Launcher pengine ndio inaonekana kuchangia sana kupakuliwa na watu wengi zaidi.
Ipo inayopatikana bure ambayo ni Nova Launcher na ya kununua inayojulikana kama Nova Launcher Prime. Uzuri wa Launcher hii ni kwamba ina mipangilio tofauti wenye ladha na muonekano mzuri kulingana na mahitaji ya mtumiaji mwenyewe.
Kwa mara ya kwanza Nova Launcher ilianza kupatikana Play Store,Septemba 10, mwaka 2013. Kama una mashaka yoyote kuhusu uzuri wa Nova Launcher unaweza kuijaribu kwa kuipakua Nova Launcher.