fbpx

Nokia kuingiza dola 3.48 kwa kila simu yenye 5G

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Mabishano kuhusiana na leseni za hakimiliki kwa kampuni za kielektroniki ni mojawapo kati ya mada moto – hasa kutokana na ukweli kuwa huibuka mara kwa mara kwenye vyombo vya habari.

Lakini sasa, Nokia na kampuni nyingine kubwa za simu zinachukua hatua mahususi kuepuka migongano katika siku za usoni kwa kutangaza hadharani ada ya leseni zinazohusiana na ubunifu wa teknolojia zao za mtandao wa 5G katika simu janja (rununu).

Gharama za leseni ya Nokia ni za aina moja tu ambazo ni dola za Marekani 3.48 (takribani sh. 7,971.29 za kitanzania) kwa kila simu itakayokuwa ya 5G duniani.

Kiwango hicho ni cha juu zaidi ya kampuni nyingine zote, lakini katika kile kinachoonekana kuwa ni matokeo ya jina lake kubwa kibiashara katika kwenye teknolojia.

Fahamu kwa uchache utengenezwaji wa simu

Uundwaji wa simu hutegemea teknolojia kutoka kampuni mbalimbali za vifaa vya kielektroniki vinavyotumika kwenye simu husika na kampuni moja pekee haiwezi kuunda iliyotakana na vipuri vyake mwenyewe kwa silimia zote.

Mwezi Juni mwaka huu, kulishuhudiwa uzinduzi wa kizio cha kimataifa cha teknolojia ya mfumo wa 5G ambapo kiujumla tutegemee ushirikiano wa pamoja kwa wataalamu na pia watafiti kutoka kampuni mbalimbali za simu zisizotumia waya zikiwemo za Qualcomm, Huawei, Ericsson, Samsung na Nokia.

Nokia kuingiza dola

Matarajio ya ongezeko la faida kutokana na kile watachokipata kutokana na teknolojia ya 5G.

Hao ndio Nokia ambao wanaonekana kutafuta kila njia ambayo itasaidia kupata mapato na hatimae kuwa kwenye ushindani wa kibiashara na makampuni mengine.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Matangazo Ya Samsung Kuwa Vifaa Vya Kuchajia Galaxy S10!
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.