Kwenye soko la ushindani ukianza kutaka simu janja nzuri, zenye kuvutia hakika Xiaomi itakuwa ni mojawapo na hii inadhihirika wakati wa takwimu za mauzo ya bidhaa zinazotoka mara nne kwa mwaka.
Nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa Xiaomi, mara zote nimekutana na rununu ambazo zinanifanya nivutiwe nazo; hii inatokana na kuweza kwenda sambamba kwa kile ambacho mteja anakihitaji. Kwa haraka haraka leo nikasema niiangalie nje ndani ya Xiaomi Mi 11X Pro. Fuata nami kuweza kuifahamu simu hii ambayo ipo sokoni tangu Mei 5.
Sifa za Xiaomi Mi 11X Pro
Kioo :
- Ukubwa: inchi 6.67
- Ubora: Super AMOLED (1080*2400px, 120Hz); ung’avu wa hali ya juu sana+umbo mithili ya tone la maji kwenye kamera ya mbele
Memori :
- Diski uhifadhi: 128GB/256 GB
- RAM: GB 8
Kamera :
- Kamera Kuu: MP 108, 8, na 5+taa moja ya kuongeza mwangaza sehemu ambazo kuna mwanga hafifu. Ina uwezo wa kurekodi picha mnato za ubora wa 8K, 4K na 1080px
- Kamera ya Mbele: MP 20+Ina uwezo wa kurekodi picha mnato za ubora wa 1080px na 720px
Betri/Chaji :
- Li-Ion 4250 mAh
- USB-C 2.0, OTG+uwezo wa kuchaji haraka kwa nguvu ya 33W (100% kwa dakika 52)
Kipuri mama :
- Snapdragon 888 5G
Uzito :
- Gramu 196
Programu Endeshi
- Realme MIUI 12, Android 11
Rangi/Bei :
- Nyeusi, Fedha na Nyeupe
- GB 8/128-$545 (zaidi ya Tsh. 1,255,432) na GB 8/256-$573 (zaidi ya Tsh. 1,318,822) bei ya India
Haina sehemu ya kuchomeka spika, nyuma/mbele kioo chake ni Gorilla Glass 5, teknolojia ya mawasiliano ni GSM / HSPA / LTE / 5G, Bluetooth 5.2, WiFi, Power Delivery 3.0, Quick Charge 3+.
Simu hii ni muendelezo wa makala zetu mbalimbali zinazohusu uchambuzi wa rununu lakini mwisho wa siku wewe ndio wa kufanya maamuzi ya kuinunua ama la! TeknoKona tunaendelea kukuhabarisha na usisite kutupa maoni yako hivyo tunasema karibu tena.
Vyanzo: Gadgets 360, GizMoChina, GSMArena
One Comment