Kulingana na taarifa ambazo zimetoka kwa watafiti na wachanganuzi kutoka katika kampuni ijulikanayo kama Sensor Tower, ni kwamba kuna ugumu katika App za kawaida kupata nafasi za juu ukilinganisha na App za magemu katika soko la App Store.
Mpaka App yoyote ishike nafasi za juu kama vile katika kumi bora kuna mambo mengi ambayo yanazingatiwa moja wapo ikiwa ni uwezo wake wa kuweza kushushwa sana.

Taarifa hizo zinasema kuwa kwa sasa inachukua mpaka ushushwaji (downloads) wa mara 156,000 kwa siku kwa App ambazo sio magemu ili kupata nafasi za juu (ya kwanza?) katika App Store.
Namba hiyo imeongezeka sana kwani kwa mwaka 2019 namba hiyo ilikua ni ushushwaji 114,000 tuu.
Vile vile hiyo namba bado ni kubwa sana kama ukisema ufananishe na mwaka 2020, kwa kipindi hicho App ambazo sio za magemu zilikua zinahitaji ushushwaji (downloads) 185,000 tuu kwa siku ili kuweza kupata nafasi za juu kabisa.
Hiyo ilikua ni ongezeko la asilimia 62 kutoka mwaka 2019 katika soko hilo maarufu la App Store.

Ukiachana na aina hizi za App vipi kuhusu zile App ambazo ni za magemu? Hapa Sensor Tower napo wakuja na taarifa.
App za magemu kwa sasa inahitaji ushushwaji (downloads) 93,000 tuu kwa siku ili kupata nafasi za juu (namba moja?) kabisa katika soko la App Store.
Namba hii imeshuka sana kwani kwa mwaka 2019 ilihitajika ushushwaji wa 171,000 ili kupata nafasi za juu katika soko.
Hii inamaanisha kuwa App za magemu ni rahisi sana kupata namba za juu ukilinganisha na App za aina nyingine.
Ukiachana na haya yote lakini kuna baadhi ya vyanzo zinasema kuwa App wao huwa hawatumii kigezo hiki tuu katika kuhakikisha kuwa wanapata orodha ya App zinazofanya vizuri.
Ningependa kusikia kutoka kwako, Niandikie hapo chini katika eneo la comment, niambie hii umeipokeaje? Unadhani kuna njia nyingine ya ziada ambayo inatumika katika kupanga orodha hii?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.