Shirika la usalama wa anga Marekani, FAA, limeshasema kwamba ndege za Boeing 737 Max zipo huru kutumika tena baada ya maboresho yaliyofanywa na kampuni ya Boeing ili kuepusha ajali nyingine tena. Ila inaonekana bado watu na makampuni kadhaa hawana haraka ya kuzitumia.
Ndege za Boeing 737 Max zilikuja zikisifika sana kwa kuweza kutumia mafuta machache zaidi, chini kwa asilimia 20 ukilinganisha na ndege zingine za ukubwa na ubora kama wake. Hivyo ni ndege iliyopendwa sana na mashirika ya safari za ndege. Ndege za 737 Max zilisimamishwa kutumika duniani kote mwaka 2019 Machi baada ya ajali za ndege hizo nchini Indonesia na Ethiopia – ajali zilitokea ndani ya kipindi cha miezi mitano na kuua watu 346.

FAA imetoa ruhusa ya ndege hizo kuendelea kutumiwa baada ya kujiridhisha juu ya maboresho ya kiusalama na kimafunzo yaliyotolewa na Boeing.
Nchini Canada, chombo kinachosimamia usafiri nchini humo, Transport Canada, kimesema itabidi wao wenyewe pia wajiridhishe ndio waruhusu kampuni yeyote inayotumia ndege hizo kuendelea kutoa huduma. Chombo hicho kinataka kujihusisha juu ya mafunzo ya marubani na hatua zingine za kiusalama zitakazokuwa zinachukulia kabla ya safari.
- Tayari ndege zaidi 470 zimefikishwa kwa wateja
- Utengenezaji wa ndege hizi ulizimwa Januari – Mei 2020, baada ya hapo ukarudi tena ila kwa kasi ndogo
- Kwa sasa bado kuna oda ya ndege zingine 4,437
- Kwa mwaka 2020 oda za ndege 640 zilivunjwa na wateja
Makampuni kadhaa tuu ata nchini Marekani ndio wameanza kuzitumia ndege hizo, bado kuna makampuni yanasubiri kujiridhisha kupitia mafunzo mbalimbali kwa marubani wake.
Kufikia mwisho wa mwaka jana tafiti zilikuwa bado zinaonesha abiria wengi wapo radhi wabadili ndege kama wakikutana na ndege hiyo wakati wa kununua tiketi. Hili suala limefanya baadhi ya mashirika ya ndege nchini Marekani kuchagua kutokuweka jina la ‘Max’ wanapozitaja ndege za Boeing 737 Max.
Kwa Marekani katika mashirika makubwa ni American Airways tuu ndio ambaye amaeshaanza kuzitumia ndege hizo huku wengine wakisema kuna taratibu zao zingine wakizimaliza kabla ya kuweza kuzitumia za kwao tena.
Wa zamani wapata habari njema, wateja wapya wa ndege mpya zaidi za Boeing 737 Max wapata matatizo mengine..
Ndege mpya za Boeing 737 zaidi ya 100 zilizotengenezwa kuanzia mwishoni mwa mwaka jana na kupelekwa kwa wateja inasemakana zinamatatizo ya mfumo wa umeme katika eneo la marubani (cockpit). Tayari Boeing wanazifanyia kazi, tatizo hilo ni la kitofauti kutokana na mabadiliko yaliyofanywa katika utengenezaji na hivyo halihusiani na ndege zilizotengenezwa na kuuzwa kabla ya katazo la utumiaji wa ndege hizo.
Je una mtazamo gani juu ya ndege hii? Tayari Boeing ashakabizisha zaidi ya ndege 470 za Boeing 737 Max kwa wateja wake, ni mbili tuu ndio zishapata ajali.
Je unadhani kama abiria na ukitakiwa kusafiri kwenye ndege hii utasifiri kwa amani?
Chanzo: ZDNET na vyanzo mbalimbali
No Comment! Be the first one.