fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Samsung simu Teknolojia Uchambuzi

Na hii ndio Samsung Galaxy M12

Na hii ndio Samsung Galaxy M12

Spread the love

Katika simu janja ambazo zimeshatoka kwa mwaka huu mpaka sasa kutoka Samsung basi mojawapo kati ya ni Galaxy M12 ambayo imeshseni sifa nyingi za kuvutia.

Samsung imekuwa moja ya kampuni ambayo inatoa simu janja katika mtiririko usio na mpangilio maalum na hivi katika hilo kwenye familia ya “M” hivi sasa kuna Galaxy M12 baada ya kuzinduliwa huko Vietnam na huu ndio undani wa rununu husika.

Kioo/Kipuri mama

SIku hizi makampuni haya yanayofanya biashara ya simu janja yanatoa rununu ambazo zina kioo kipana; Galaxy M12 ina ichi 6.5 cha ubora wa PLS LCD, 720px+ za ung’avu lakini si hapo tuu kwani kufanya ufanisi wa ufanyajiu kazi uende vizuri umewezeshwa na Exynos 850.

SOMA PIA  Google Kuanza Kutengeneza "Chip" Zao Kwa Ajili ya Android

Kamera/Betri

Siku hizi simu janja n yingi zinawezeshwa kamera ambazo zitafanya picha/picha mnato kuwa na ubora wa hali ya juu jambo ambalo limesababishwa na ukuaji wa teknolojia. Simu hii ina jumla ya kamera nne (4) nyuma, taa ya kuongeza mwanga na moja upande wa mbele. Kamera kuu ina MP 48 yenye uwezo wa kurekodi picha jongefu katika ubora wa 1080px, MP 5 ambayo inaweza kupiga mpicha mpaka za nyuzi 123, MP 2 mbili zenye za kupata picha nzuri za kitu kilicho mbali na kidogo. Kamera ya mbele ina MP 8.

Upande a betri simu husika ina 6000mAh, 15W ambapo inadumu kwa chaji saa 24 kama utatumia kuperuzi mtandaoni tu kupitia WiFi, saa 23 ukiangalia picha jongefu pekee ama siku 5 iwapo utaitumia kusikiliza muziki.

Galaxy M12

Inatumia USB Type-C, OTG.

Memori

SOMA PIA  Kigogo wa Samsung aliyehukumiwa jela miaka 5 aachiwa huru

Hapa ni moja ya kipengele ambacho wateja wengi ulimwenguni kote wanapenda kujua na hii inatokana na ukweli kwamba siku hizi vifaa vya kidijiti ni msaada kwa masuala mengi tuu mbali na kuwezesha mawasiliano. Daima tufahamu kuwa ufanisi mzuri wa simu unachagizwa na ukubwa wa memori kuu (RAM). Kwenye simu ina GB 3, 4 na 6 za RAM, GB 64/128 diski uhifadhi lakini pia uwezo wa kumeka memori ya ziada mpaka TB 1.

Bei/Mengineyo

Sim hii inapatikana kwa bei tofauti tofauti kutokana na kwamba kuna toleo la India na nyingine kwa soko la Ulaya. Bei ya chini kabisa kwa ile ya 4/64GB toleo la India ni $149|zaidi ya Tsh. 344,471, 6/128GB ikiuzwa kwa $190|zaidi ya Tsh. 438,426 gharama za ughaibuni, rangi ni Nyeusi, Kijani na Bluu na nguvu ya betri ni 6000mAh.

SOMA PIA  Apple Waacha Kutengeneza Tena iPhone 12 Mini!

Zile ambazo zimetoka mahususi kwa ajili ya bara la Ulaya wezo wa betri ni 5000mAh, RAM GB 3/4, diski uhifadhi GB 32, 64 na 128 ikiwa na uwezo wa kuongeza memori ya ziada mpaka TB 1, bei uake ikianzia $465|zaidi ya Tsh. 1,069,753 kwa 4/64GB.

Galaxy M12

Matoleo ya soko la India na Ulaya zina sehemu ya kuchomeka spika za masikioni, teknolojia ya kutumia alama ya kidole kwa pembeni, Bluetooth 5.0, inatumia kadi mbili za simu.

Haya sasa ewe msomaji wetu ni wewe wa kufanya maamuzi ipi ya kununua kutokana na sababu mbalimbali ila kumbuka kama utainunulia Tanzania basi bei yake itakuwa juu.

Vyanzo: Gadgets 360, GSMArena

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania