fbpx

Samsung

Mwenyekiti wa Samsung Lee Kun-hee amefariki akiwa na umri wa miaka 78

mwenyekiti-wa-samsung-lee-kun-hee-amefariki

Sambaza

Mwenyekiti wa Samsung Electronics Lee Kun-hee, mtu aliyefanikiwa kuijenga kampuni ya Samsung hadi kufikia kiwango cha mafanikio amefariki dunia akiwa na miaka 78.

Mwenyekiti wa Samsung Lee Kun-hee amefariki
Mwenyekiti wa Samsung Lee Kun-hee amefariki

 

Bwana Lee, ambaye wakati wa kifo chake alibaki kuwa mwenyekiti wa kampuni hiyo, alikuwa amelazwa hospitalini tangu Mei 2014 baada ya mshtuko wa moyo kumwacha akiwa amelemazwa. Tayari alikuwa na afya dhaifu na alitibiwa saratani ya mapafu mwishoni mwa miaka ya 1990.

  • Lee alizaliwa huko Daegu, Korea inayomilikiwa na Wajapani, mnamo Januari 9, 1942.
  • Aliifanya Samsung kuwa kubwa duniani kupitia bidhaa zao za simu, luninga kumpyuta, vipuri vya vifaa elektroniki na biashara zingine mbalimbali.
  • Lee alichukua kampuni hiyo mnamo 1987 baada ya kifo cha baba yake na mwanzilishi wa Samsung, Lee Byung-chul.
  • Aliongoza Samsung kuja kuwa kampuni kubwa dhidi ya makampuni pinzani ya Marekani na ya kijapani.

Data za mwaka 2017 zinaonesha kampuni ya Samsung Group kwa pamoja ilichangia asilimia 17 ya mapato ya taifa la Korea Kusini.

INAYOHUSIANA  Simu za Samsung zinazouza kwa sana India - Samsung Galaxy J6 & J8
samsung electronics
Kampuni ya Samsung ni moja ya makampuni makubwa duniani

 

Soma habari za Samsung -> Teknokona/Samsung

Mnamo 1996, Lee alihukumiwa kwa kumuhonga rais wa Korea Kusini, lakini kisha akasamehewa, Times iliripoti. Miaka kadhaa baadaye, Lee alihukumiwa kwa kukwepa kulipa kodi lakini alisamehewa tena ili aweze kusaidia Korea Kusini kushawishi kuleta Olimpiki za msimu wa baridi katika mji wa milima wa Pyeongchang mnamo 2018.

Kwa kiasi kikubwa ataendelea kukumbukwa katika taifa hilo kama moja ya watu muhimu waliokuwa na mchango mkubwa wa kusaidia maendeleo ya kiuchumi kwa taifa la Korea Kusini. Na hili ndilo limeweza kumsaidia ata kuzishinda skendo kadhaa ambazo zilimkuta katika miaka ya hivi karibuni.

Vyanzo: Reuters na vyanzo mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags:

Dennis Dealma

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*