fbpx
Infinix, simu

Simu Janja Mpya Kutoka Infinix: Jua Sifa Za Infinix S5!

mpya-kutoka-infinix-infinix-s5
Sambaza

Hivi unalikumbuka tolea la S4 kutoka simu za Infinix?  Naam! Ni moja kati ya yale matoleo yanayotoka katika  ‘S Series’ . Hivi Sasa kampuni ya Infinix inakuletea toleo lingine linalojulikana kama Infinix S5. Simu hii imekuja sambamba na msimu wa sikukuu hivyo tegemea promoseni ambayo ina zawadi kedekede kutoka kwao Infinix

Ijulikane kwamba kwa sasa Infinix S5 ndio kinara wa matoleo ya ‘S Series’ kutoka Infinix, simu janja hii ina vipengele vya kuvutia kama vile ‘Infinity-O Display’ na Megapixel (MP) 32 katika kamera yake ya selfi.

“Infinix ikiwa ni kampuni yenye ushawishi mkubwa katika mfumo wa kidigitali tunawahakikishia wateja wetu bidhaa zenye teknolojia ya hali ya juu kwa bei Rafiki”- alisema afisa mahusiano Infinix, Aisha Kurupa

Timu Ya Infinix Ikizindua Simu Janja Ya Infinix S5
Timu Ya Infinix Ikiwa Kazini

SIFA ZAKE KWA UFUPI

  • Kamera ya selfi ambayo ina MP 32
  • Kamera nne za nyuma ambazo ni 16MP+5MP+2MP+AI Lens vile vile zikiwa na teknolojia ya Artificial Inteligency (AI)
  • Memori ya uhifadhi wa ndani ni Gb 64 na RAM ni GB 4 kwa ujazo huu simu yako haitawahi kujaa mafaili kwa haraka ila ikitokea unaweza ukaongezea memori kadi ya nje.
  • Betri yake ina ujazo wa mAh 4,000. Ujazo huu utaiwezesha simu janja hii kukaa na chaji kwa muda mrefu sana.
INAYOHUSIANA  Sifa za Undani - Simu ya Tecno Phantom 6
Timu Ya Infinix Ikizindua Simu Janja Ya Infinix S5
Timu Ya Infinix Ikizindua Simu Janja Ya Infinix S5

Infinix S5 ina sifa nyingi sana, pia inakuja katika muonekano wa kitofauti sana wenye kuvutia kutokana na namna kamera ya mbele ilivyopachikwa ndani ya Display kwa jina la kitaalamu Infinity-O Display. S5 pia inakuja na uwezo wa laini mbili za simu zile ndogo kabisa.

Ukiachana na hayo Infinix wametumia nafasi hiyo kutambulisha rasmi promosheni ya msimu wa sikukuu inayoenda sambamba na uzinduzi wa Infinix S5.

Akizungumza meneja wa mauzo wa Infinix Bwana Fredy Kadilana alisema kwamba, “katika msimu huu wa sikukuu za Christmas na mwaka mpya Infinix imezindua rasmi promotion itakayompa nafasi mteja wa Infinix S5 au mteja wa simu yoyote ya Infinix kujishindia zawadi mbalimbali kama vile Vacuum Cleaner, Deep Flyer, Subwoofer Radio na nyengine nyingi lakini pia Infinix haijasahau wadau wake wa wanaotembelea kurasa ya @infinixmobiletz kwa kuitambulisha challenge ya #S5showitoff itayoanza rasmi mwishoni mwa wiki hii”.

Muonekano Wa Infinix S5 Ndani Ya Boksi

Kwa maelezo zaidi tembelea www.infinixmobility.com

INAYOHUSIANA  Vodacom Waja na Ofa Kabambe!

Ningependa kusikia kutoka kwako, hili kutoka Infinix umelipokea vipi? niandikie hapo chini sehemu ya maoni. Pia Usisit kutemnelea katika mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila siku kwa habari kedekede za sayansi na teknolojia kwa ujumla.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com