fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
IPhone Picha

Mpaka iPhone 5s Imechukua Tuzo Ya Picha Bora 2021! #IPPAWARDS

Mpaka  iPhone 5s  Imechukua Tuzo Ya Picha Bora 2021! #IPPAWARDS

Spread the love

Tuzo za zinazojulikana kama  IPPAWARDS zimefanyika kwa mwaka 2021 na iphone 5s imeshinda moja kati ya picha bora (iliyopigwa na simu hiyo).

Hii ni ya kushangaza sana kwani iPhone 5s ilizinduliwa mwaka 2013 na mpaka sasa inatimiza miaka nane sasa inawezekana vipi simu hiyo ishinde kama mpigaji picha ya mwaka?

SOMA PIA  Miaka 30 ya mafaili ya mtindo wa GIF. - Fahamu historia yake!

Kumbuka simu nyingi sasa hivi tumeziozea zikitoka mpaka na kamera tatu na nyingine zikiwa zinakuja na kamera nyingi kuliko hizo.

Ukiachana na hayo kwa iPhone tuu kuna mabadiliko mengi, yaani yale ya hardware na hata software kwa iPhone hizi mpya ukilinganisha na iPhone 5s ya mwaka 2013.

Picha Iliyopigwa Na iPhone 5s Na Kuchukua Moja Ya Tuzo Ya Picha Bora 2021

Picha Iliyopigwa Na iPhone 5s Na Kuchukua Moja Ya Tuzo Ya Picha Bora 2021

Katika tuzo hizi unaweza dhani kuwa kuna matoleo mengi mapya ya simu ambazo zimechukua tuzo. Ni kweli kuna picha 54 ambazo zimechukua tuzo hizi.

SOMA PIA  Thamani ya kava la simu ya Messi ni 50M za kitanzania!

Cha kushangaza ni kwamba kati ya hizo 47 zilipigwa na simu za zamani ukiachana na 7 tuu ambazo zilikua zimepigwa na iPhone 12 au iPhone 12 Pro Max.

47 ya picha hizo zimepigwa na iPhone X, iPhone XR, and the iPhone 7, na simu zingine zingine. Pia ukitaka kuona list ya simu ambazo zimechukua ushindi ingia –> HAPA <—

SOMA PIA  Apple kuzuiwa kuuza iPhone 6 na 6 Plus Nchini China Kisa Wizi wa Ubunifu

Ningependa Kusikia Kutoka Kwako, Niandikie Hapo Chini Katika Eneo La Comment, Hii umepokeaje?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kwani Daima Tupo Na Wewe Katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania