fbpx

simu, Teknolojia

Motorola One nyingine kutoka Mei 15

motorola-one-kutoka-mei-15

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Sambaza

Tangu mwezi Machi 2019 taarifa kuhusu sifa za simu janja, Motorola One zimekuwa zikienea lakini simu hiyo itajulikana kwa uwazi kabisa hapo Mei 15 huko San Paulo-Brazil kulingana na tangazo rasmi.

Ingawa tarehe rasmi kuhusiana na uzinduzi wa simu imeshawekwa wazi lakini pia sifa kuu ambazo wateja wa simu wanapenda kuzijua tayari zimekwishafahamika kilichobaki ni kutaka kujua nyongeza au kwa lugha nyingine sifa za ndani kidogo. Baadhi ya vipengele ambavyo udnani wake unajulikana ni kama ifuatavyo:-

SOMA PIA  Kamera ya Megapixel 23, Kioo cha 4K: Ifahamu SONY XPERIA Z5 PREMIUM

Kipuri mama. Ufanisi wa simu unategemea sana na nguvu/aina ya kipuri mama ambacho kimewekwa kwenye simu husika na kwa muujibu wa vyanzo mbalimbali imefahamika kuwa simu husika imewekwa Exynos 9610 SoC.

Kioo/Muonekano. Kioo cha simu husika kinaelezwa kuwa na urefu wa inchi 6.2 chenye ung’avu wa hali ya juu ambapo hakuna umbo la herufi “V” lakini kamera ya mbele imewekwa upande wa kushoto ikionna ama shimo dogo ambalo huwezi kulihisi kwa ukigusa kamera husika.

SOMA PIA  Jinsi ya Kufungua WhatsApp kwa Haraka Zaidi kwenye Kompyuta
Motorola One
Muonekano wa mbele na nyuma- Motorola One

Memori ya ndani/RAM. Upande wa Memori Motorola wameamua kuweka matoleo tofauti tofati kwa RAM pamoja na didki uhifadhi; RAM ni ya kiwango cha GB 3 au GB 4 huku memori ya ndani ni GB 32, GB 64 au GB 128.

Kamera. Watu wengi na wapenzi wa simu janja wanapenda rununu (simu janja) ambayo ina uwezo mkubwa kwenye kipengele hiki na kwa simu husika upande wa nyuma una kamera mbili huku kamera kuu ina 48MP.

SOMA PIA  Teknolojia ya FaceID kuruhusu uso mmoja tu kusajiliwa

Nguvu ya betri/Mengineyo. Betri lake lina 3500mAh huku sehemu ya kuchaji ikitumia USB-C, inatumia Android Pie. VIlevile, ina teknolojia ya kutumia alama ya kidole iliyowekwa upande wa nyuma.

Kuweza kufahamu mengi zaidi ambayo bado hayajafahamika na ni muhimu kuyajua tuwe na subira mpaka hapo itakapozinduliwa Mei 15 mwaka huu. TeknoKona kama kawaida yetu jicho letu huwa haliachi kufuatilia teknolojia.

Chanzo: GSMArena

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|