Kampuni ya Tesla imeanza uzalishaji wa magari ya bei naafu ya umeme yanayokwenda kwa jina la Model 3, Elon Musk ambaye ndiye mkurugenzi mtendaji ameonesha picha za gari ya kwanza katika mlolongo wa aina hii ya magari.
Gari hilo la umeme ambalo ndio la gharama ya chini linategemewa kuuzwa kwa karibu shilingi milioni 80 za kitanzania, hii ni karibu nusu ya bei ambayo gari la Model S kutoka Tesla. Model 3 ni gari ambalo linategemewa kutembea kilomita 300 baada ya kuchajiwa mara moja, hii inategemea na uendeshaji wa dereva.
Soma Pia: Ufaransa kupiga marufuku magari yanayotumia diseli na petroli.
Tesla inategemea kufanya sherehe ya kuwagawia magari hayo wateja wake wa kwanza 30 ambayo itafanyika baadae mwezi huu, hata hivyo bado kuna wasiwasi wa muda ambao wateja waliokwisha lipia magari hayo wataweza kupewa magari yao. Tesla imesema kwamba wateja wanao agiza magari hayo wameongezeka maradufu, inakisiwa kwamba mwezi Agosti magari 100 yatatengenezwa wakati kwa mwezi Septemba magari 1,500 yanategemewa kutengenezwa kwa mwezi huo.
Hii ni habari kubwa kwasababu magari ya umeme yaliyokuwa yanatengenezwa siku za nyuma yalikuwa ghari zaidi, lakini hii ni habari njema zaidi kwa wanamazingira ambao wamekuwa wakipigania teknolojia rafiki na mazingira.