fbpx

Mkakati wa kuachana na magari yanayotumia mafuta waanza nchini Uingereza

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Katika hali ya kukabiliana na hali ya hewa chafu inayosababishwa na magari yanayotumia dizeli/petroli Uingereza nayo imeonekana kufuata nyayo za Ufaransa. Mwisho ni mwaka 2040 kwa magari yanayotumia mafuta huko Uingereza.

Moja kati ya vitu ambavyo vimekua vikiathiri mabadiliko ya tabia ya nchi duniani kote ni hewa chafu zinazozalishwa na viwanda, uchimbaji wa madini, n.k ikiwemo uchafu unazalishwa kwenye magari yanayotumia mafuta.

INAYOHUSIANA  Samsung ya Ujerumani imetoa memori kadi ya 512GB

Magari mapya yanayotumia mafuta ya diseli na petroli nchini Uingezeza yataandolewa barabarani kuanzia mwaka 2040 kama njia ya kukabiliana na uchafuzi wa hewa.

Katika kuonyesha nia thabiti ya kukabiliana na hewa chafu itakonayo na magari yanayotumia mafuta Mawaziri watazindua ufadhili wa pauni milioni 255(zaidi ya $332 milioni) kusaidia kukabiliana na gesi chafu kutoka kwa magari yanayotumia dizeli ikiwa ni sehemu ya pauni bilioni 3 za kusaidia kusafisha hewa.

kuachana na magari yanayotumia mafuta waanza nchini Uingereza

Kuachana na magari yanayotumia mafuta waanza nchini Uingereza: Baada ya kesi mahakamani serikali iliamrishwa na mahakama kubuni mipango mipya na kutangaza viwango vipya vya uchafuzi wa hewa huku hatua za mwisho za mipango hiyo ikitarajiwa kukamilika Julai 31.

Ni wazi kwamba hatua hiyo itakuza sana mahitaji ya magari yanayotumia umeme na hivyo kufanya uhitaji wa magari hayo kuongezeka. Iwapo mtu bado atakuwa anahitaji kumiliki gari inayotumia mafuta basi atalipisha kiasi kikubwa cha fedha.

INAYOHUSIANA  Ndege za bila ya rubani/drones kusimamiwa zaidi Uingereza

Je, unadhani kwa nchi zetu za Afrika tunakaribia kuachana na matumizi ya magari yanayotumia mafuta na mbadala wake kuwa magari yanayotumia umeme? Tupe maoni yako.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.